23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

ANSAF kukutanisha wadau wa kilimo Dodoma

Na MWANDISHI WETU

JUKWAA la wadau wa Kilimo Wasio wa Kiserikali (ANSAF), imeandaa mkutano wa mwaka wa kujifunza na kubadilishana uzoefu baina ya wadau utakaofanyika jijini Dodoma Desemba 3 na 4 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa ANSAF, Audax Rukonge amesema tukio hilo litawakutanisha pamoja wadau takribani 200 wakiwakilisha taasisi mbalimbali, mashirika ya umma na binafsi, wizara, watafiti na wataalamu kutoka taasisi za elimu ya juu, makampuni, wazalishaji, vijana waliojikita kwenye shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi.

 Amesema mkutano huo umebeba ajenda inayosema “Kufungua Fursa za Ajira kwa Vijana Katika Kilimo Kupitia Uchumi Wa Viwanda”.

“Ajenda hii imeambatana na ajenda zingine ndogo tatu nazo ni kubainisha maeneo ya fursa kwa vijana kujiajiri na kuajiri wengine kwenye sekta ya kilimo kupitia viwanda: Mada hii ndogo imekusudiwa kuchambua kiundani uhusiano kati ya sekta za viwanda na kilimo ili kubaini kwa kina maendeleo ya kilimo kwa masilahi ya wazalishaji wadogo maeneo ya vijana kuanzia ama kuingilia(kujikita) katika kilimo biashara kwa ajili ya ajira na uzalishaji wa kipato,”amesema.

Amesema ajenda nyingine ni upatikanaji wa masoko ndani, kikanda na kimataifa, ambapo watajadili namna ambavyo Tanzania inaweza kubaini fursa za masoko ya kikanda kulingana na kiasi cha uzalishaji nchini na kujadili changamoto zilizopo na kutoa mapendekezo yakihusisha fursa za ajira kwa vijana kwenye sekta ya kilimo.

“Pia kubainisha huduma na taasisi zake ambapo mada hii italenga kujadili juu ya masuala upatikanaji wa huduma za kifedha na rasilimali zingine zinazomwezesha kijana kufanya uzalishaji wenye tija.

“Vilevile inalenga kutathimini mazingira wezeshi ya watoa huduma yanaathiri vipi suala la ajira kwa vijana katika minyororo ya thamani ya kilimo kupitia maendeleo ya viwanda,”amesema.

Rukonge amesema wanaamini kwamba uchumi wa viwanda ni chachu ya kutengeneza fursa za ajira kwa vijana na kuchangia kukua kwa uchumi wa nchi.

“Endapo tataamua kubadilisha mtazamo na kutengeneza miundombinu bora na mazingira wezeshi kwa vijana kujikita kwenye sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi,”amesema Rukonge

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles