25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Anne-Marie Lewis – Si kazi ngumu mwanamke kuwa rubani

Anne-Marie LewisNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

LICHA ya kwamba uwepo wa wanawake katika sekta ya usafiri wa anga kuwa mdogo, uwezo wa kuwa viongozi katika usafiri wa anga hauna mwiko. Akizungumza na gazeti hili, rubani mwanamke wa kwanza kuongoza ndege aina ya Airbus A380 inayomilikiwa na kampuni ya Fastjet Tanzania, rubani Anne-Marie Lewis anasema wanawake barani Afrika hawapaswi kuogopa kuwa sehemu ya sekta hii inayokua barani kote.

Anasema si kazi ngumu mwanamke kuwa rubani na kwamba yeye anajiamini na hana woga katika jambo lolote lile ndio maana akaaminiwa na kupata fursa ya kungoza ndege hiyo katika mikoa ya Tanzania na nchi nyingine za jirani.

“Wanawake wanapaswa kuelewa kwamba  hakuna aina ya kazi ambayo ipo kwa ajili ya wanaume peke yao, bali wanawake wataleta katika sekta ya usafiri wa anga uwezo wao wa kufanya kazi kwa bidii, kulea na ujuzi wao wa usimamizi bora,” anasema.

Kwa mujibu wa Lewis, wanawake wa Afrika wanahitaji kuelewa kwamba nia na uamuzi wao utaondoa hofu au hasara ya kiuchumi. Anasema uwezo wao wa kufanya kitu chochote, ambapo wataweka mawazo yao juu ya kile wanachotaka kukifanya utakuwa ndio msukumo wa malengo yao.

Anabainisha kuwa yeye alianzia chini kabisa lakini nia yake ya kuingia katika hii fani iliyokuwa imetawaliwa na wanaume na kwa msaada wa mara kwa mara kutoka kwa  baba yake ulikuwa ndio msingi wa mafanikio anayoyapata mpaka sasa.

Vijana wengi barani Afrika wanaweza kufikiri kwamba wao ni kundi lisilokuwa na faida, lakini wanapaswa kufurahi kwa sababu wako katika maisha ya kisasa ya kidigitali hivyo wanaweza kutumia kujifunza chochote wanachotaka.
Rubani Lewis anasema  wanawake wanapotaka kuondokana na umaskini hukumbwa na changamoto nyingi, hii ni kwa sababu wanaonekana ni watu wa kukaa na kusubiri kuletewa na waume zao.

“Ili kufanikiwa, wanawake wanatakiwa wawe wao kama wao… wanaleta sifa za kipekee katika nafasi yoyote kwa kuwa wao ni wasikivu wazuri, walezi na wana ujuzi mkubwa wa kupangilia mambo,” anasema na kuongeza kuwa nia, msukumo na shauku daima hutoa kilicho bora, pia ni msingi wa mafanikio.

Aidha, Lewis anatoa pongezi kwa baba yake akisema; “baba yangu alijua alipaswa kuongoza kwa mfano, kutuonyesha sisi kwamba ili kufanikiwa inahitaji kufanya kazi kwa bidii na nia.”
Anaongeza kuwa baba yao aliwasisitiza wasichana wote juu ya umuhimu wa elimu kwa kuwa ndio njia ya kuwa huru kiuchumi.

“Wanawake wa Afrika wanao uwezo wa kufanya kazi katika eneo lolote la sekta ya anga. Kama mimi nilivyo rubani, napenda kuona marubani wanawake zaidi Tanzania, ambao watakuwa wakitoa mafunzo kwa marubani wanaowasimamia. “Wataleta mabadiliko katika sekta za anga sawa na wale wanawake wa magharibi walioleta mabadiliko katika sekta za anga katika bara lao,” anahitimisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles