Murray, ambaye anashika nafasi ya pili kwa ubora wa mchezo huo duniani, ametolewa katika mzunguko wa tatu kwa seti 6-7, 6-4, 6-3, sawa na alama (1-7).
Katika mchezo huo Murray, mwenye umri wa miaka 28, alianza kwa kasi ya juu na kumtisha mpinzani wake kwa kuwa hadi mapumziko nyota huyo alikuwa akiongoza kwa seti moja.
Lakini Dimitrov ambaye ana umri wa miaka 26, alirejea uwanjani huku akionekana kuwa na mipango mipya ya ushindi na kufanikiwa kumtupa nje mpinzani wake.
“Mchezo ulikuwa na ushindani wa hali ya juu na lazima mmoja ashinde na mwingine aweze kuyaaga mashindano, nimekosa bahati ya kusonga mbele kutokana na mpinzani wangu kufanikiwa kutumia nafasi.
“Lakini ninaamini nitajifunza kutokana na makosa ambayo nimeyafanya katika michuano hii, pia nampongeza mpinzani wangu kwa kunipa changamoto kubwa na kufanikiwa kusonga mbele na namtakia kila la heri,” alisema Murray.