26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Ibrahimovic atangaza kustaafu soka

zlatanPARIS, UFARANSA

MSHAMBULIAJI wa timu ya PSG, Zlatan Ibrahimovic, amewashangaza mashabiki wengi wa soka baada ya kutangaza kwamba anaweza kustaafu soka katika kipindi cha majira ya joto.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34, mwanzoni mwa wiki hii alithibitisha kwamba baada ya kumalizika kwa msimu huu atajiunga na klabu kubwa nchini England, lakini juzi mchezaji huyo amesema kwamba anaweza kustaafu soka baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi.

Mkataba wa mchezaji huyo na klabu yake ya PSG unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini hadi sasa bado hajafanya mazungumzo juu ya mkataba mpya.

“Chochote kinaweza kutokea baada ya kumaliza mkataba wangu na PSG majira ya joto, naweza kustaafu soka langu kwa kuwa hadi sasa hakuna ambaye anajua lolote juu ya maisha yangu ya baadaye zaidi ya mimi mwenyewe, naweza kuamua kuachana na soka,” alisema Ibrahimovic.

Mchezaji huyo amekuwa na mchango mkubwa katika klabu yake na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Ufaransa msimu huu, hivyo kuzifanya klabu mbalimbali nchini England kuvutiwa na nyota huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles