26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 5, 2024

Contact us: [email protected]

Ampata mtoto aliyamtafuta miaka 24

Shandong, China

Raia wa Nchini China, Guo Gangtang amekutana na mtoto wake wa kiume baada ya miaka 24 kupita tangu alivyotekwa nyara na watu wasiojulikana nchini humo.

Raia huyo aliyesafiri umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 500,000 kwa pikipiki nchini humo kwaajili ya kumtafuta mtoto wake huyo wa kiume aliyetekwa na watu wawili mbele ya nyumba yake katika jimbo la Shandong.

Inaaminika kuwa nchi ha china kuna biashara haramu ya binadamu ambayo imepelekea msanii mkubwa wa filamu nchini humo, Andy Lau kutengeneza filamu yenye maudhui ya utekwaji nyara kwa watoto mwaka 2015.

Kutekwa nyara kwa watoto ni tatizo kubwa nchini Uchina, huku maelfu ya watoto wakiibiwa kila mwaka, kulingana na Wizara ya usalama wa umma ya Uchina, polisi waliweza kumpata mtoto huyo kwa kutumia kipimo cha vinasaba -DNA.

Pia baada ya mtoto huyo kutekwa nyara mwaka 1997, Bw Guo alirirpotiwa kusafiri zaidi ya majimbo 20 kote nchini Uchina nyuma ya mwendesha pikipiki akifuata taarifa alizopewa na watu za mahala anakoweza kuwa mtoto wake.

Katika mchakato huo, alivunjika mifupa katika ajali za barabarani na kukabiliana na wezi huku pikipiki 10 pia ziliharibika.

Akitembea na bango la picha ya mwanae wa kiume, inasemekana ameishi akiweka akiba kwa ajili ya kumtafuta mwanae, akilala chini ya madaraja, na kuomba pesa alipoishiwa.

Wakati akimsaka mwanae, pia amekuwa mjumbe maalum wa mashirika ya watu waliopotea nchini Uchina, na amesaidia wazazi takribani saba kuwapata watoto wao waliotekwa nyara.

Mara taarifa kwamba mtoto wa Bw Guo amepatikana ilipotangazwa, mitandao ya habari ya kijamii ya Uchina ilifurika kwa ujumbe wa kumsifu baba huyo.

Nchini Uchina, utekeji nyara na usafirishaji haramu wa watoto wachanga umekuwa tatizo kwa miongo mingi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles