24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

ALPONCE SIMBU: NATAKA KUANZIA PALE NILIPOISHIA

NA MARTIN  MAZUGWA


MASHINDANO ya jumuiya ya Madola yanatarajia kuanza kutimua vumbi Aprili 4 na kufika tamati tarehe 15 mwaka huu huko nchini Australia huku Tanzania ikiwa ni miongoni mwa mataifa shiriki.

Licha ya kushiriki mashindano haya kufanyika mara kwa mara lakini nchi ya Tanzania imekuwa haifanyi vizuri  jambo ambalo limekuwa likiwafanya mashabiki wa mchezo wa riadha kupungua hapa nchini tofauti na miaka ya nyuma ambapo mchezo huo ulikuwa ukipendwa sana.

Jumla ya mataifa 52 yatashiriki mashindano haya ambayo yanahusisha nchi zile yamekuwa yakiongezeka mvuto kadiri siku zinavyozidi  kwenda.

Baadhi ya watanzania waliowahi kung’ara katika mashindano hayo na kutwaa medali ya dhahabu ni Gidamis Shahanga aliyeshika nafasi ya kwanza mara mbili  mwaka 1978 na 1982, Filbert Bayi ambaye  alishinda mwaka  1974  huko Nigeria na kuwatoa kimasomaso Watanzania waliokuwa na shauku ya medali ya dhahabu.

Mara ya mwisho Tanzania kufanya vizuri katika mashindano ya jumuiya ya madola ilikuwa mwaka 2006 ambapo mwanariadha, Samson Ramadhan alipoibuka kidedea na kushika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo yaliyokuwa na upinzani mkubwa.

Ni miaka 12 hadi sasa tangu Ramadhan alipowapa medali Watanzania lakini hivi sasa wamekuwa wasindikizaji katika mashindano hayo ambayo mwaka huu yamekuwa na Tangu hapo Tanzania

Nchi yenye medali nyingi za mashindano hayo ni wenyeji Australia ambapo tangu mashindano hayo yalipoanzishwa hadi sasa wametwaa jumla ya medali 2,218 wakifuatiwa na Canada waliojikusanyia 2,008 na England ikishika nafasi ya tatu kwa kubeba mara 1,473, haya yakiwa ndio mataifa  yaliyoweka rekodi ya kujitwalia medali nyingi zaidi.

Alponce Felix Simbu (Tanzania)

Mwanariadha huyo ameomba kuondolewa katika kikosi cha Tanzania kitakachoenda kushiriki mashindano ya madola nchini Australia  akiomba aachwe ili apate muda zaidi  wa maandalizi ya michuano ya London Marathon inayotarajiwa kufanyika  Aprili 20 nchini England.

Simbu alisema kuwa lengo la kuomba hivyo anataka aanzie pale alipoishia mwaka uliopita na kusawazisha makosa ili aweze kurudi na medali ya dhahabu na kufuta ufalme wa Wakenya ambao wamekuwa wakitawala  katika mashindano mbalimbali .

“Unajua mashindano yaliyopita nilikuwa siwajui vizuri wapinzani wangu lakini mara baada ya kuwaona katika kipindi kilichopita  na kugundua madhaifu yao pamoja na makosa  yangu ni wakati wa kufanya vizuri sasa,” alisema Simbu.

Alisema kuwa kwa muda mrefu kiu yake kubwa ni kurejesha heshima ya mchezo wa riadha ndio sababu hivi sasa amekuwa akijifua mara mbili kwa siku ili kuhakikisha anakuwa katika kiwango bora kwa muda wote akiwa anayasubiri mashindano hayo.

Mkali huyo ambaye ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania  wa kwanza kushika nafasi ya tano katika mashindano ya Olimpiki mara ya mwisho kubeba medali ilikuwa mwaka 2017 aliposhika nafasi ya tatu katika mashindano ya London Marathon.

Lakini pia nyota huyo anatarajiwa kuungana na wanariadha wengine wawili katika safari yake ya mwaka huu ambapo nyota huyo mwaka uliopita alikuwa Mtanzania pekee aliyeshiriki mashindano hayo ambayo yalizidi kumpa uzoefu wa kutosha katika michuano ya Kimataifa.

Katika kuonyesha kuwa wanataka kurudisha hadhi ya mchezo wa riadha tayari wanariadha wengine wameongezwa katika safari ya Simbu ambayo hii  ni neema nyingine katika tasnia ya riadha nchini Tanzania kwani utazidi kufungua wigo zaidi kwa vijana ambao wamekuwa na ndoto ya kufikia alipo nyota huyo.

Ukiacha Simbu wafuatao ni baadhi ya wanariadha ambao pia waliwahi kuahirisha kushiriki mashindano ya madola kutokana na sababu tofauti tofauti.

Soh Rui Yong (Singapore)

Mwanariadha huyo raia wa Singapore naye anaungana na Simbu mwaka huu kwa kuomba aachwe,  amethibitisha kutoshiriki mashindano hayo ambayo yanahusisha mataifa yaliyokuwa koloni la Uingereza ambapo nyota huyo amesema hatoweza kushiriki michuano hiyo.

Mkali huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema kuwa amechukua uamuzi huo binafsi wiki iliyopita kuwa michuano hiyo haipo kwenye mipango yake kwa kipindi cha hivi karibuni.

Soh, amesema kuwa hivi sasa akili yake ipo kwaajili ya mashindano ya dunia ya nusu Marathon Championships yanayotarajia kuanza kutimua vumbi mwezi machi mwaka huu hivyo hatoweza kupata muda zaidi wa kujiandaa na mashindano ya jumuiya ya madola alikiambia kituo cha habari cha Times cha nchini humo.

“itakuwa kazi ngumu kwa kocha na wanariadha kuandaa mipango mipya kwaajili ya kufuzu vigezo na kuchukuliwa kwenda kushiriki mashindano hayo ya jumuiya ya madola,” anasema mwanariadha huyo.

Jonny Mellor(England)

Mwanariadha raia wa England , Jonny Mellor aliamua kuwaweka wazi viongozi wa chama cha riadha nchini humo  kuwa wasimjumuishe katika kikosi  chao kinachoenda kushiriki  mashindano ya Jumuiya ya madola mwaka 2017 kutokana na kupungua kwa uwezo wake wa kuona mbali akiwa anafanya mazoezi.

Nyota huyo alichukua maamuzi hayo mara baada ya kukimbia kwa sekunde 63 walipokuwa kwenye mchujo wa kutafuta wanariadha wenye vigezo vya kuiwakilisha Uingereza katika michuano hiyo.

England hawakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na maamuzi yake hivyo wakalikata jina la mwanariadha huyo aliyelazimika kubaki nyumbani na kuwashuhudia wenzake wakiipeperusha bendera  ya nchi yao katika mashindano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles