Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Mwimbaji wa Injili mwenye asili ya Cameroon anayeishi Marekani, Alexis Emile, amewaomba mashabiki wa muziki kuipokea kazi yake mpya, Yesu Amaade Nson.
Akizungumzia wimbo huo wa kusifu na kuabudu, Alexis Emile anasema ni saa na majira ya kumwabudu Mungu katika roho na kweli na anaamini mashabiki wengi wataguswa na wimbo huo ambao tayari unapatikana kwenye mitandao mbalimbali.
“Mungu anatafuta watu wanaomwabudu katika roho na kweli, nashukuru tayari nimeachia wimbo Yesu Amaade Nson katika chaneli yangu ya YouTube hivyo naomba mashabiki waendelee kubarikiwa,” amesema Alexis.
Alexis Emile ni mwanamuziki wa Injili kutoka Cameroon ambaye makazi yake ni Marekani aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia wimbo “Mud De Bahd” alioutoa mwaka 2014.
Mwimbaji huyo kutoka familia ya Kikristo, alijibu wito wa Mungu wa kutumia sauti ya dhahabu kueneza habari njema ya Mungu kupitia muziki kwa nyimbo kama Miracles, Finally, Jehova Oye, Happy Sunday, Mega Things, Dry Bones This Life na sasa Yes Amaade Nson. Pia Alexis Emile ameoa na amebarikiwa kuwa na watoto wawili wa kiume.