24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

ALBERT EINSTEIN: KUTANA NA KILAZA ALIYEIBUKA KUWA NGULI WA FIZIKIA – 2

Mtaalamu wa magonjwa ya damu (pathologist), Thomas Harvey akionyesha ubongo wa Albert Einstein.

Na Joseph Lino


WIKI hii tunaendelea na historia ya mwanasayansi maarufu Albert Einstein aliyeleta mapinduzi katika ulimwengu wa sayansi ambapo enzi za utoto wake walimu walimwita kilaza darasani.

Maisha ya awali ya Eistein hayakukubalika kwa walimu kutokana kutokuwa na akili darasani. Juhudi zake binafsi katika kuamini anachokifanya kilimfanya kuwa ‘genius’ yaani mtu mwenye uwezo wa akili wa kiwango cha juu yaani IQ (Intelligence Quotients-160-190).

Einstein alianza kujulikana katika masuala ya Fizikia na umaarufu wake ulizidi kuongezeka kutokana na tafiti zake kukubalika, hatua  ambayo ilizifanya kazi zake kupata sifa kem kem katika ulimwengu wa Fizikia.

Akiwa  nchini Ujerumani, kipindi hicho chuki dhidi ya Wayahudi iliongezeka, Einstein alianza kupata mashambulizi kutoka kwa wanasayansi wenzake Philipp Lenard na Johannes Stark ambao walikuwa washindi wa tuzo za Nobel katika masuala ya Fikizia.

Wanafizikia hao walianza kuhusisha nadharia ya Einstein kuwa ‘fizikia ni Kiyahudi.’ (Theory of Relativity) hivyo, mwanasayansi huyu alijiuzulu kutoka Chuo cha Prussia cha Sayansi mwaka wa 1933.

Kwa mara kadhaa, Einstein alikuwa akitembelea Chuo cha California Institute of Technology nchini Marekani, ambapo safari yake ya mwisho mwaka 1933 alipewa nafasi katika Institute for Advanced Studies huku Princeton, huko Massachusetts.

Akiwa nchini Marekani, mwaka 1939 Einstein alikuwa mstari wa mbele katika utengenezaji wa bomu la atomiki, alimuandikia barua aliyekuwa Rais wa Marekani wakati huo, Franklin D. Roosevelt kuelezea kuwa Wajerumani wamepiga hatua katika maendeleo ya sayansi, kwamba Adolf Hitler anaweza kuwa wa kwanza kutengeneza silaha za atomiki.

Hii ilichochea jitihada za Marekani kutengeneza bomu la nyuklia. Einstein alishtuka na kusikitishwa kutokana fumbo maarufu la Fikizia E = mc 2 ambalo lilionyesha njia ya kutumia katika kutengeza bomu la nyuklia ambalo lililolitumika kulipua mji wa Hiroshima nchini Japan, mwaka 1945.

Einstein alifariki Aprili mwaka 1955 kwa maradhi ya tumbo. Kabla ya kufariki, aliomba mwili wake uchomwe moto, lakini tukio la kushangaza mtaalamu wa magonjwa ya damu (pathologist),  Thomas Harvey aliondoa ubongo wakati mwili wake ukifanyiwa uchunguzi. Harvey alichukua ubongo ili kutafuta siri ya kiwango cha akili yake (genius).

Baada ya kupata kibali ambacho kilikuwa kinakataliwa kutoka kwa mtoto wa kiume wa Einstein, Harvey baadaye aliukata ubongo wa Einstein vipande vipande na kuupeleka kwa wanasayansi mbalimbali kwa ajili ya uchunguzi. Tafiti kadhaa zimefanyika kuhusiana na ubongo wake tangu miaka ya 1980, lakini matokeo yake yamekuwa yakikataliwa au kutopewa heshima yoyote.

Lakini mwaka 1999, uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha Canada ilichapisha utafiti wenye utata unaodai Einstein alikuwa na ukuta usio wa kawaida katika sehemu ya ubongo uliompa uwezo wa Hisabati.

Wakati Albert Einstein anaendelea kutengeneza fedha nyingi, ingawa alifariki mwaka 1955; mwaka huu jarida la Forbes lilimtaja katika nafasi ya 10 kuwa miongoni mwa watu waliokufa lakini wanaendelea kuzalisha fedha. Einstein mwaka huu pekee amezalisha Dola za Marekani milioni 10 kutokana na jina na sura yake kutumika katika bidhaa, mabango, kompyuta, roboti na mifuko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles