25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

ALBERT EINSTEIN: KILAZA ALIYEIBUKA KUWA NGULI WA FIZIKIA

Na Joseph Lino


ALBERT Einstein ni mwanasayansi maarufu aliyeleta mapinduzi katika ulimwengu wa sayansi ambapo enzi za utoto wake walimu walimwita kilaza darasani.

Maisha ya awali ya Eistern hayakukubalika kwa walimu kutokana kutokuwa na akili darasani. Juhudi zake binafsi katika kuamini anachokifanya kilimfanya kuwa ‘genius’ yaani mtu mwenye uwezo wa akili wa kiwango cha juu cha Intelligence Quotients- IQ (160-190).

Msomi huyu ambaye alianza kama mjinga, aligeuza ujinga wake kuwa mwanasayansi mashuhuri na katika historia ya duniani hatoweza kusahaulika.

Mwanafizikia huyu raia wa Marekani mwenye asili ya Ujerumani, alifanya mapinduzi ya sayansi ya fizikia, anajulikana zaidi kwa kugundua sayansi ya mabomu ya nyuklia.

Einstein alizaliwa mwaka 1879, huko Ulm, Ujerumani, alipata elimu ya awali katika mji wa Munich. Alikuwa mwanafunzi mwenye kiwango cha akili kidogo baadhi ya walimu wake walidhani kuwa  ni walemavu wa akili (mentally handicapped); kutokana na kushindwa kuzungumza vizuri alipokuwa na umri wa miaka tisa.

Hata hivyo, alivutiwa na masuala ya asili ya ulimwengu. Alikuwa na  hisia za ajabu ya kushangaza na aligundua kuwapo kwa nguvu isiyoonekana (Invisible forces) inayoongoza sindano ya dira (campass).

Alipokuwa na umri wa miaka 16 aliweza kufanya mahesabu ya kutatua na kufumbua  masuala ya fizikia na uhandisi.

Einstein alimaliza elimu ya sekondari  akiwa na miaka 16 na hakupenda kuendelea na masomo, akaamua kuachana nayo na kusoma mwenyewe huku akitafuta njia ya kuingia chuo kikuu.

Mwalimu wake akamfukuza kwa sababu ya mtazamo wake ambao ungeweza kuwaathiri wanafunzi wa darasa lake.

Einstein alijaribu kutuma maombi ya kujisajili na chuo cha Federal Institute of Technology (FIT) huko Zurich nchini Uswisi, lakini ujuzi wake wa masomo yasiyo ya hisabati hakuwa na uwezo nayo hivyo kusababisha kufeli mtihani wa kujiunga na chuo hicho.

Kwa ushauri wa mkuu wa chuo, alienda kujiunga na chuo cha  Cantonal huko Aarau, Uswisi na kufanikiwa kupata diploma ambayo ilimwezesha kukubaliwa na chuo cha FIT mwaka 1896 ambapo alishindwa awali.

Akiwa hapo, alitambua uwezo wake mkubwa katika masuala ya fizikia kuliko hisabati.

Einstein alifaulu na kuhitimu katika chuo cha FIT mwaka 1900, lakini kwa sababu ya kutoelewana na mmoja wa profesa wake hakuweza kuendelea masomo kutokana na kukosa msaada wa fedha.

Mwaka 1902, aliajiriwa katika chuo cha Bern akiwa mkaguzi, nchini Uswisi, lakini baada kufikisha umri wa miaka 26 alitimiza vigezo vyote vya kumwezesha kufundisha chuo kikuu. Aliandika utafiti wake  wa kwanza kuhusu mapinduzi ya sayansi.

Utafiti huo ulimpa umaarufu Einstein, na vyuo vikuu vikaanza kumgombania kwa huduma zake, mwaka 1909, baada ya kutumika kama mwalimu wa chuo cha Bern aliitwa kufanya kazi akiwa profesa msaidizi wa Chuo Kikuu cha Zurich huko Uswiss. Miaka miwili baadaye alichaguliwa kuwa profesa kamili katika Chuo Kikuu cha Ujerumani huko Prague, nchini Czechoslovakia. Ndani ya  mwaka mmoja na nusu akarudi katika chuo cha FIT akiwa profesa kamili.

Hatimaye, mwaka 1913, wanasayansi maarufu wa Max Planck na Walther Nernst walisafiri kwenda Zurich kumshawishi Einstein kukubali kuwa profesa wa Chuo Kikuu cha Berlin huko Ujerumani, pamoja kuwa mwanachama kamili wa Chuo cha Sayansi cha Prussia ambapo alikubali hiyo ofa.

ITAENDELEA WIKI IJAYO

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles