ALBAMU mpya ya mwanamuziki Kanye West, ya ‘Life of Pablo’ inaongoza kwa kusikilizwa bila malipo yoyote.
Albamu hiyo yenye siku nne tangu ilipoachiwa imeshaangaliwa mara 500,000 katika mtandao wa Torrent Freak, wakati mwenyewe alidai inauzwa kwenye mtandao mmoja wa Tridal.
Hata hivyo, maelfu ya watu waliolipa ili kusikiza albamu hiyo walilalamika kutoipata mtandaoni, licha ya kuilipia.
“Nashangaa kuona albamu hiyo ikisambaa zaidi tofauti na mafanikio ninayopata, naamini kuna wizi unafanyika,” aliandika Kanye kwenye akaunti yake ya twitter.