30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Al-Shabaab yawaua 24 wakitazama mechi ya Man United

Al-ShababBAIDOA, SOMALIA

WATU 24 wameuawa mjini Baidoa, kusini mwa Somalia wakitazama mechi ya Ligi Kuu nchini England kati ya Manchester United dhidi ya Arsenal kwa shambulio la kigaidi ambalo lilifanywa na Al-Shabaab.

Taarifa za awali zilieleza kwamba, milipuko miwili mikubwa ilitokea katika mgahawa maarufu mjini humo ambao ulikuwa umejaa mashabiki wengi wa mechi kati ya Manchester United na Arsenal.

Hata hivyo, inadaiwa kwamba miongoni mwa wale waliouawa ni pamoja na ofisa mmoja wa serikali ya jiji hilo.

Inasemekana kwamba mji wa Baidoa ulitekwa na wapiganaji wa Kiislamu wa Al-Shabaab mwaka 2008, lakini walifukuzwa mwaka 2012.

Mji huo ulioko takriban kilomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu, ni mji ambao umekuwa ukishambuliwa na wanamgambo hao wa Kiislamu.

Shambulizi la kwanza lilitokea katika mgahawa maarufu unaopendwa na wageni na viongozi wa kisiasa ambao ulishambuliwa kwa gari lililokuwa limetegwa bomu, lakini watu walinusurika na kifo.

Hata hivyo, mwishoni mwa wiki iliyopita watu wengine zaidi ya 20 waliuawa katika mgahawa mwingine kufuatia shambulizi la Al Shabaab.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles