32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Al Ahly wahaha kuisoma Yanga

Al-Ahly-vs-Yanga*Yakiri ugumu wa kupata michezo iliyocheza karibuni

NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

WAPINZANI wa Yanga katika michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri, imekiri kuwa na ugumu wa kupata michezo ya timu hiyo ili kusoma mbinu wanazotumia.

Yanga inatarajia kuvaana na Waarabu hao katika mchezo wao wa hatua ya 16 bora unaotarajiwa kuchezwa Aprili 10 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kurudiana kati ya Aprili 19 hadi 20 Misri.

Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Al Ahly, Syed Abdul Hafiz amethibitisha ugumu wa kupata michezo ya Yanga katika mtandao wa klabu hiyo.

Abdul Hafiz alisema kwamba Ubalozi wa Misri nchini Tanzania uliwahakikishia kupata mikanda hiyo lakini siku chache zilizopita waliwatumia taarifa za kushindwa kupata kanda hizo zinazohusisha mchezo wa awali wa Yanga dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius na ule wa APR ya Rwanda, kwakuwa michezo hiyo haikuonyeshwa katika televisheni yoyote.

Mkurugenzi huyo alieleza, tayari ameanza kutuma ujumbe kwa  maofisa wa Ubalozi wa Rwanda, ili kupata kanda za video za  mchezo wa Yanga dhidi ya APR uliochezwa Machi 12 katika Uwanja wa Amahoro, ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

 

Hata hivyo, hatua hiyo ya kuhamishia nguvu Rwanda, imekuja baada ya kushindikana juhudi za kipelelezi zilizokuwa zikifanywa na Balozi wa Misri nchini, Yesser Shawwaf.

Machi 22 mwaka huu Balozi Shawwaf alimuahidi mkurugenzi huyo kumtafutia mikanda hiyo ili kuisadia timu hiyo kufahamu mbinu za udhaifu wa Yanga.

Hata hivyo, maofisa wa timu hiyo wanatarajia kutua nchini wakati wowote, kuangalia jinsi gani watapata hoteli nzuri na nafuu hapa nchini watakayofikia, uwanja wa mazoezi pamoja na usafiri wa ndani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles