26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Akili Karafura: Waimbaji tunaoishi Marekani tuache ubinafsi

BOISE IDAHO, MAREKANI

JAMHURI ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), imeendelea kuzalisha wanamuziki wengi ambao hufanya kazi zao ndani na nje ya bara la Afrika, mfano ni Akili Karafura, kipaji kipya cha muziki kinachokuja kwa kasi kutoka nchini Marekani.

Akili ambaye tayari ameachia ngoma kibao kama vile Sodoma, Ni Mwaka Wako, Nitapona, Mshukuru Mungu, Dunia, Uko Yahweh na Ngangana Na Wewe, amefanya mahojiano na Swaggaz kama ifuatavyo.

Swaggaz: Changamoto zipi unakutana nazo unapofanya muziki wako nje ya Afrika?

Akili: Changamoto kubwa ninayokutana nayo ninapofanya audio nakosa ile ladha ya Kiafrika ambayo siipati huku Marekani, inabidi ufanye audio nyumbani Afrika kwa sababu wazungu huku hawapigi biti za Kiafrika, kwa hiyo inabidi utumie maprodyuza kutoka nyumbani wanaoendana na tamaduni za Kiafrika pia changamoto ipo kwenye video kwa sababu ‘location’ hapa Marekani zipo nyingi mpaka tunachanganyikiwa ila hatuna ‘directors’ wakubwa wa kuweza kutuongoza tufanye mambo makubwa.

Maana ukimwambia mzungu akufanyie video anaweza kuacha vitu vingi sana maana ukimpa aidia ya video ya tamaduni ya Afrika anaweza asielewe lakini pia kipindi cha baridi huwa kunakuwa na barafu sana kwahiyo video zinashindikana kufanyika.

Swaggaz: Waimbaji gani wa Afrika hasa Tanzania unatamani kufanya nao kazi?

Akili: Kwa Tanzania ambao nawakubali sana na ninaona Mungu anafanya kazi ndani yao ni mchungaji Abiudi Misholi huyu mzee anaimbaga vizuri sana, Rose Muhando ni mama ninayempenda sana na Bahati Bukuku ni mama mstaarabu na mnyenyekevu.

Swaggaz: Kwanini umeamua kufanya gospo na sio muziki wa kizazi kipya kama vijana wengine?

Akili: Mimi sifanyi gospo ili nipate pesa, nafanya gospo ni kuonyesha ukubwa wa Mungu, Kwa sababu Mungu aliponitoa na kunichunga hapa Marekani lazima nimuinue, siwezi na sipendi kuimba nyimbo za Bongo Fleva za kumsifia mapenzi, nahitaji kuwa karibu na utukufu wa Mungu ambaye anatupa uzima bure  kwahiyo lazima tumshukuru.

Swaggaz: Tukio gani huwezi kulisahau kwenye safari yako ya muziki?

Akili: Siwezi kusahau ile watu walikuwa hawanikubali  pia unakuta unafanya kitu na mtu kama kufungua huduma lakini anakuwa anakuibia na kukuzunguka.

Swaggaz: Tabia gani huipendi kwa waimbaji wenzako hapo marekani?

Akili: Waimbaji wa hapa Marekani wana ubinafsi wa kufanya kazi wenyewe, hawapendiu kutambulisha waimbaji wengine, mtu akiona amefanikiwa hapendi mtu mwingine afike hiyo sehemu, ni jambo linaloniuma sana kwa sababu muziki huu ni kwaajili ya kumtukuza Mungu.

Unaweza pata tamasha fulani, lazima uite wenzako mshirikiane kutumbuiza na kumtumikia Mungu, lazima tupendane na kuungana mkono kwa kila jambo.

Swaggaz: Mapokezi ya wimbo wako mpya Ngangana Na Wewe yapo vipi?

Akili: Mapokezi sio mabaya, nashukuru Mungu ametupa hicho kibali, kwa sababu mimi mwenyewe nilipitia magumu mengi ndio ikabidi niachie hiyo ngoma kwa sababu napaswa kushikilia Yesu kila siku. Marafiki wapo Norway, Sweden, Canada, Finland, Australia na kwingineko wananiupigia simu kwamba wanafurahia wimbo wangu.

Swaggaz: Kwa mashabiki zako wapya watarajie kutoka kwa Akili?

Akili: Nina mpango wa kuachia nyimbo mbili mfululizo, zitakuwa nyimbo kali sana za kumtumikia Mungu na milango ikifunguka ninaandaa tamasha langu inaweza kuwa Oktoba au Novemba mwaka huu ya kuzindua albamu yangu. Naweza kuleta wasanii hata wawili kutoka Afrika ya kuja kutumbuiza huku nitamkatia tiketi aje huku Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles