29.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 21, 2022

Gigy Money, mpenzi wake wazichapa

 CHRISTOPHER MSEKENA 

UGOMVI wa msanii Gift Stanford ‘Gigy Money’ na mpenzi wake mwenye asili ya Nigeria, Hunchy Huncho, mbele ya waandishi wa habari usiku wa kuamkia jana unatajwa kuwa ni wivu wa mapenzi. 

Ugomvi huo ulitokea wakati wa hafla ya tamasha la msanii mpya wa WCB, Zuchu Kopa lililojulikana kwa jina la IAM Zuchu (Asante Nashukuru) na kufanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City. 

Gigy Money alikuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza kutumbuiza, lakini ugomvi huo unadaiwa kutokana na Gigy Money kumtoroka mpenzi wake, hivyo mrembo huyo alimpiga mpenzi wake na kiatu huku jamaa huyo akitaka kuvua shati ili azichape vizuri jambo lililofanya mabausa waingilie kati ugomvi huo na kuwatenganisha. 

Aidha, mastaa kibao walihudhulia onyesho hilo la kwanza la Zuchu, wakiongozwa na Diamond Platnumz, Wema Sepetu, Hamisa Mobetto, Haji Manara, Juma Jux, Rayvanny, Mbosso, Lavalava, Millen Magese, Irene Uwoya, Lady Jay Dee, Flaviana Matata na wengine kibao huku mgeni rasmi akiwa ni Dk Hassan Abbaz, Katibu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
191,701FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles