FREDRICK KATULANDA Na PETER FABIAN-UKARA
WANAFUNZI 47 wa shule za msingi za sekondari, ni miongoni mwa watu waliofariki dunia kwenye ajali ya kivuko cha Mv Nyerere kilichozama Septemba 20 kikiwa kimebakiza mita 50 kitie nanga kwenye gati la Kijiji cha Bwisya kisiwani Ukara.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Boniface Magembe, alisema kati ya wanafunzi hao, wanaosoma shule ya msingi ni wanafunzi 24 ambako mwili wa mwanafunzi mmoja bado haujapatikana.
Magembe alisema katika ya wanafunzi hao 24, wanafunzi wa shule ya Msingi Bwisya ni 14 na wanafunzi wa shule za sekondari ni 13.
DC Magembe alisema mbali na wanafunzi hao, watumishi wa Serikali ambao walifariki dunia katika ajali hiyo ni sita.
“Bado tunaendelea kufuatilia iwapo miili mingine itapatikana, lakini mpaka sasa watumishi wa kada mbalimbali ambao tunajua wamepoteza maisha ni sita,” alisema.
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.