24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Airtel na TPB Bank waungana kupata suluhisho huduma za Fedha kidigitali nchini

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzani imetangaza kuiingia ubia na Benki ya TPB kwa lengo na dhamira ya kuboresha na kupanua wigo wa huduma za kifedha nchini.

Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money imekua ikitoa huduma mbalimbali za kifedha kwa njia ya mtandao ikiwemo kutoa na kupokea pesa popote, kulipia Ankara mbalimbali kama vile LUKU, DSTV, malipo mbalimbali ya serikali, huduma za Maji kama Dawasco na nyingine nyingi.

Mkurugezi wa huduma za kimtandao Jema Msuya kutokaTPB benki akiongea jijini Dar es Salaam wakati akitangaza ubia baina ya Airtel ba Benki ya TPB ambapo Wateja wa Airtel Money sasa watakuwa na uhakika kufanya miamala yao kwa uhakika  wakiwa popote kama vile kuhifadhi au kutoa pesa toka benki ya TPB kwenda moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money ili kufanya malipo mbalimbali ya huduma kama vile LUKU, Ankara za Maji, DSTV, au kukamilisha malipo mbalimbali ya tozo za serikali. Kulia ni Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda

Akiongea wakati wa Mkutano maalum na waandishi wa habari wakutangaza Ubia kati ya Airtel na TPB benki, Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda amesema ubia huo utasaidia kuboresha huduma kwa mawakala na wateja wa huduma hizo.

“Ubia tunaoingia hapa leo utasaidia sana kuboresha huduma tunazotoa kwa kuwafaidisha zaidi mawakala wetu wa Airtel Money waliopo kila mahali nchini ambapo benki ya TPB imefika.

“Pia wateja wa Airtel Money sasa watakuwa na uhakika kufanya miamala yao kwa uhakika kabisa wakiwa popote kama vile kuhifadhi au kutoa pesa toka benki ya TPB kwenda moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money ili kufanya malipo mbalimbali ya huduma kama vile LUKU, Ankara za Maji, DSTV, au kukamilisha malipo mbalimbali ya tozo za serikali,” amesema Nchunda.

Aidha, Nchunda ameelezea kuwa; “Mawakala sasa hawana haja ya kubeba bulungutu la fedha na kusafiri umbali mkubwa kupata salio au (Float), sasa watahudumiwa kwenye tawi lolote la TPB karibu yake, Hii itasaidia sana kwenye kuokoa muda na fedha ambazo walizitumia kama nauli kwenda umbali mrefu ili kupata salio/Float, sasa ni haraka zaidi na salama.,” amesema.

Amesema ubia wao na Benki ya TPB unalengo la kuendeleza ubunifu katika utoaji wa huduma za fedha kiditali kwa kupunguza madhara yanayowakumba mawakala au wateja wetu wanaposafiri umbali mrefu kufata huduma, sasa watajiunga na benki ya TPB karibu yao na kufanya miamala yote kigitali kupitia Airtel Money kwenda benki au kutoka benki kwenda Artel Money.

“Muunganiko wetu utaendelea kukamilisha dhamira yetu tuliyojiwekea sisi wabia ya kutoa huduma nafuu, kwa haraka, bila mipaka ili kikidhi mahitaji ya wateja wetu ya kila siku,” amesisitiza Nchunda.

Akiongea kwa niaba ya TPB benki Mkurugezi wa huduma za kimtandao, Jema Msuya amesema; “TPB tunaaamini suluhisho la huduma za kifedha katika utoaji huduma unatija sana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi, hivyo basi Ubia wetu na Airtel ni muendelezo wa kuendelea kupunguza changamomoto za pande zote yaani za wale waliofikiwa na huduma za kibenki na ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki popote walipo kwa kuwa sasa watapata huduma kwa njia ya mtandao na kufanya malipo kidigitali. 

“Benki ya TPB kila tuponakuja na huduma yenye ubunifu zaidi lengo letu ni kuongeza au kutoa suluhisho zaidi kwa wateja wetu pamoja na kuwapatia huduma kwa unafuu huku tukizingatia ubora zaidi. Ubia wetu na Airtel Money leo hii unadhihirisha dhamira yetu hiyo ya kutoa huduma kabambe, zenye usalama bila kuzingatia mipaka yaani huduma popote ulipo. Kila mteja wetu anaweza kujipatia huduma zetu akiwa na simu yake kiganjani kutokana na ubia huu sasa,” amesema Msuya.

Kwa mujibu wa Airtel ili wakala au Mteja aweze kupata huduma hii ya  atatakiwa kutembeleia tawi letu la TPB bank na kujaza fomu maalum ya huduma bila kupoteza wakati ataanza kufurahia huduma zetu kwa kupiga *150*60# cahagua namba  0 Ongeza Pesa Select 2 Hamisha toka Benki
Select 4 TPB Benki na ufuate maelekezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles