25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Ahoua mchezaji bora

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kiungo wa Simba, Jean Charles Ahoua amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara wa mwezi Agosti, huku Kocha Mkuu wa timu hiyo Fadlu Davids akichaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi huo.

Ahoua ameibuka kidedea kutokana na mchango wake uliwezesha timu kupata ushindi katika michezo miwili ya ligi hiyo, huku akifunga bao moja na akitoa ‘asisti’ tatu.

Kwa upande wake amewashinda Patrick Aussems wa Singida Black Stars na Abdalah Mohamed ‘Bares’ wa Mashujaa alioingia nao fainali baada ya kocha huyo raia wa Afrika Kusini kuiongoza Simba kuvuna pointi sita katika mechi mbili ilizocheza ikifunga mabao saba.

Aidha, kamati ya tuzo imemtangaza meneja wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Ashraf Omary kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Agosti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles