26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Agathon Rwasa atengwa katika siasa

BUJUMBURA, BURUNDI

SERIKALI ya Burundi imekataa kusajili chama kipya cha siasa cha National Liberty Front kilichoanzishwa hivi karibuni na kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, Agathon Rwasa.

Mwanasiasa huyo alianzisha chama cha National Liberty Front au Amizero y’Abarundi, baada ya kupitishwa kwa mabadiliko ya katiba mwezi Mei mwaka huu ambayo yanakataza muungano wa wagombea binafsi kushiriki kwenye uchaguzi.

Licha ya mara kadhaa Rwasa kuonekana kutokuwa mpinzani wa kweli kwa chama tawala cha CNDD-FDD, muungano wake wa Amizero y’Abarundi ulipata asilimia 17 ya kura katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Hivi karibuni, Rwasa, mwanasiasa mkongwe na mashuhuri wa upinzani nchini Burundi, alisema itawalazimu wanasiasa wa upinzani kujizatiti katika vyama vyao ili baadaye kujiweka pamoja wakati wa mpambano wa uchaguzi kwa mujibu wa katiba mpya.

Kwa sasa Rwasa ni Makamu Spika wa Bunge na alikuwa akiwakilisha mseto wa vyama vya upinzani wa Amizero y’Abarundi.

Muungano huo katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2015 ulishika nafasi ya pili ukitanguliwa na chama tawala CNDD FDD cha Rais Pierre Nkurunziza.

Rwasa amewahi kuishi uhamishoni katika nchi jirani ya Tanzania kwa takribani miaka 20 alipotoroka uongozi wa Watutsi wachache. Rwasa alitoroka tena Machi mwaka 2010 wakati CNDD FDD ikiongoza kabla ya kurejea Burundi mwaka 2013.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles