30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Afya ya Mufti Zubeir yazidi kuimarika

shkhNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

AFYA ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir bin Ali, imezidi kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo kwenye  Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyoko Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Neema Mwangomo, alisema hata hivyo bado Mufti Zubeir amelazwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu zaidi.

“Tunamshukuru Mungu, afya ya Mufti Zubeir inazidi kuimarika, lakini bado amelazwa hapa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi na madaktari wake,” alisema.

Mufti Zubeir alifikishwa hospitalini hapo mwishoni mwa wiki, akiwa ameongozana na ndugu zake pamoja na baadhi ya waumini wa dini hiyo.

Taarifa iliyotumwa juzi na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kwa vyombo vya habari, ilisema Mufti Zubeir alifanyiwa upasuaji  wa tumbo kutokana na matatizo yaliyokuwa yanamsibu, japo hayakuwekwa hadharani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles