KABOUL, AFGHANISTAN
NCHI ya Afganistan imeelezwa kuwa ni hatari kwa uhai wa wanawake wanasiasa Shuhra Koofi alikuwa na wasiwasi. Mama yake ambaye amekuwa mbunge nchini Afganistan kwa mihula miwili, alikuwa amepigwa risasi alipokuwa akisafiri kurudi mjini Kabul kwa gari.
Shuhra alimsihi mama yake, Fawzia Koofi, asifunge macho yake ‘’nitafanya nini bila wewe?
‘’Nilikuwa nina hofu kwa sababu nilidhani nimempoteza mama yangu,’’ Shuhra aliiambia BBC, kuhusu jaribio la mauaji mwezi uliopita. ‘’Lakini baadae nikajikaza kwa kuwa alikuwa akihitaji msaada wangu.’’
Fawzia Koofi ni mkosoaji mkubwa wa Taliban katika meza ya mazungumzo. Amekutana na athari kubwa kutokana na kujihusisha na siasa.
Mwaka 2010, msafara wake ulivamiwa na Taliban, na mwezi Agosti mwaka huu alipigwa risasi barabarani na watu wasiojulikana
Agosti 14, mwaka huu, Shushra na mama yake walikuwa wakirejea mjini Kabul baada ya kuzuru jimbo la Parwan, Kaskazini mwa mji mkuu wa Afghanistan ndipo walibaini kulikuwa na magari mawili yaliyokuwa yakiwafuata.
‘’Kabla ya shambulio, gari jeusi lilituzuia na dereva wetu alipiga honi ,’’ Shuhra alisema.’’ Kisha tukasikia milio ya risadi kutokea nyuma-upande aliokuwa amekaaa mama yangu.’’ Kulikuwa na risasi mbili, Shuhra alisema. Ya kwanza iliikosa gari yao.
Shuhra alikuwa amekaa karibu na Fawzia kwenye kiti cha nyuma. Alijaribu kumkinga kichwa mama yake na kumwambia abonyee chini ya kiti wakati dereva akikimbiza gari. Hakuwaona washambuliaji.
‘’Ilitupasa kuondoka kabisa vinginevyo wangetushambulia tena,’’ alisema.
Shuhra akiwa amemtembelea mama yake hospitali baada ya kushambuliwa mwezi uliopita
Mwaka 2010 , Fawzia na Shuhra walikuwa wakisafiri mwenye gari kupitia Nangarhar jimbo lililo Afghanistan . Fawzia tayari alikuwa mmbunge na mshirika wa karibu wa Rais wa kipindi hicho , Hamid Karzai.
‘’Nilikuwa na miaka 10 wakati huo. Nilikuwa nakaa kwenye gari katikati ya mama yangu na dada yangu,’’ Shuhra alisema. Ninakumbuka kelele za risasi. Zilikuwa za mfululizo.’’
Fawzia alinusurika na tukio hilo na polisi waliusindikiza msafara mpaka kwenye eneo salama ambapo walipanda ndege kuelekea Kabul.
‘’Ilikuwa rahisi kukubali hilo kwa sababu tulijua ni nani anayehusika,’’ Shuhra alisema. ‘’ Mara ya pili, washambuliaji hawakufahamika na hakuna aliyekuwa akiwajibika, hiyo ilikuwa ngumu zaidi na ilikuwa ikiiweka familia katika hofu kubwa.’’