28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

ACT wajipanga kupinga muswada wa sheria mbalimbali bungeni

Mwandishi wetu, Dar es Salaam

CHAMA Cha ACT Wazalendo, kimesema kimeshtushwa na hatua ya Serikali kupeleka bungeni muswada wa marekebisho ya sheria ambao kimedai utazuia taasisi zisizo za kiserikali kufungua mashauri ya kikatiba kwamba kimemuagiza Mbunge wake, Zitto Kabwe, kwenda bungeni kuupinga.

Taarifa kwa umma ya chama hicho iliyotolewa jana ilisema muswada huo unakusudia kuzuia taasisi zisizo za kiserikali kufungua mashauri ya kikatiba lakini pia kumkingia kifua Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mku, Spika wa Bunge, Naibu Spika wa Bunge na Jaji Mkuu dhidi ya mashitaka ya uvunjaji wa Katiba, huku pia ukiweka vikwazo kwa watu binafsi kufungua mashauri hayo.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Omar Said Shaaban, ilisema muswada huo pia unaweka sharti la mtu binafsi kuonesha ni kwa namna gani vitendo vya uvunjaji wa Katiba vimemuathiri yeye binafsi.

Ilisema Serikali inakusudia kurekebisha sheria ya The Basic Rights and Duties Enforcement Act (Cap. 3), The Law Reform (Fatal Accident and Mscellaneous Provisions) Act (Cap. 310).

Ilisema Serikali inapeleka marekebisho hayo ikijua wajibu wa kuhifadhi na kuilinda katiba na sheria za nchi una maana pana na wajibu huo haupo kwa watu binafsi bali hata kwa taasisi na mashirika bila ya kujali kuwa uvunjifu wa Katiba unaathari binafsi kwao ama la.

“ Msingi huu wa Kisheria umewekwa vizuri sana kwenye Uamuzi wa Jaji Mlacha wa tarehe 18.03.2020 kwenye Shauri la Zitto Zuberi Kabwe dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano na wengine.

“Chama cha ACT Wazalendo kinayatazama marekebisho haya kama ni muendelezo wa Serikali kuziwekea vikwazo jithada za raia na taasisi zisizo za kiserikali dhidi ya vitendo vya uvunjwaji wa Katiba na sharia za nchi.

 “Chama cha ACT Wazalendo kimemuagiza mbunge wake (Zitto) kwenda kupinga marekebisho haya bungeni na kuwashawishi wabunge wengine wenye nia njema na nchi kuyapinga kwa kuwa hayana maslahi kwa Taifa.” ilisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles