26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

ACT: CCM imechangia kuporomoka kwa uchumi

Kamati Kuu ya chama cha ACT Wazalendo imetoa maazimio juu ya hali ya nchi baada ya kukaa kwa siku mbili katika kikao chake cha Kawaida ambapo ilipitia hali ya Kisiasa na kiuchumi nchini pamoja na Bara la Afrika kwa ujumla.

Akiwasilisha maazimio hayo leo Juni 11 mbele ya waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya chama hicho Magomeni jijini Dar es Salaam, Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe amesema moja ya maazimio waliyofikia ni kasi ya ukuaji wa uchumi kuporomoka kutokana na Serikali ya CCM ya awamu ya tano chini rais John Magufuli kukata nishati ya kuendesha uchumi.

“Takwimu za benki Kuu ya Tanzania zinaonyesha kuwa kwa mwaka unaoishia Machi 2018 urari wa biashara kati ya Tanzania na nchi nyingine duniani ulikuwa hasi kwa dola bilioni 2, Kwa mwezi unaoishia Machi 2019 urari wa biashara umetanuka kufikia hasi ya dola bilioni 2.5 sawa na ongezeko la dola milioni 500,” amesema.

“Hata taasisi kama benki ya dunia wamezuia fedha kuja nchini, fedha ambazo zimezuiliwa ni pamoja na ambazo zinapaswa kufadhili miradi ya kuboresha elimu ya sekondari SEQIP dola milioni 400 sawa na shilingi bilioni 920, TASAF III dola za kimarekani milioni 300 sawa na shilingi bilioni 660 na mradi wa Maji Vijijini wenye thamani ya dola milioni 300,

“Fedha hizi zimezuiwa Kwa sababu ya Serikali kutunga sheria kandamizi ya takwimu kwa lengo la kuwadhibiti wakosoaji wa Serikali wanaotumia ushahidi wa takwimu lakini madhara yake kwa nchi ni makubwa mno,” amesema

“Sababu nyingine ni uminywaji wa demokrasia nchini, msingi wake mkuu ukiwa ni kuporwa kwa ushindi wa Maalim Seif Sharif Hamad Katika Uchaguzi mkuu wa Zanzibar 2015, kuzuia Bunge Live, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vya upinzani  wakati ya CCM ikiruhusiwa na kuwabambikia kesi mbalimbali wanasiasa wa upinzani, kupigwa risasi kwa Mbunge Tundu Lissu akiwa kwenye eneo la Bunge, na Kutungwa kwa sheria mpya ya vyama vya siasa inayoua kabisa siasa za vyama vingi nchi,” amesema.

Ameongeza kuwa Kupungua kwa Uwekezaji nchini (FDI) kunapekelea shughuli za Uchumi kutoongezeka, kutozalisha ajira rasmi za kutosha na kutoongeza mapato ya Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles