25.5 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Acheni kuweka watu ndani kwa saa 48- RC Kagaigai

Na Upendo Mosha,Moshi

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kagaigai amewaagiza Wakuu wapya wa Wilaya kuacha matumizi mabaya ya kutumia sheria za kuweka watu kizuizini kwa saa 48 na badala yake kuitumia vema na kwa haki.

Pia amewaagiza wakuu hao wa wilaya, kudhibiti mianya ya wizi na ubadhirifu katika Halmashauri zao kwa kufuata misingi na miongozo ya sheria.

Kagaigai alitoa maagizo hayo leo Jumanne Juni 22, 2021 wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya wa mkoa huo, ofisini kwake mjini Moshi, ambapo amesema kuwa baadhi ya wakuu wa wilaya wamekuwa wakiitumia sheria hiyo vibaya jambo si sahihi.

Amesema hatafurahishwa na baadhi ya wakuu wa wilaya ambao wataitumia sheria hiyo vibaya kwa makosa ambayo yanaweza kushughulikiwa na Mkuu wa polisi wa wilaya (OCD).

Amesema baadhi ya wakuu wa wilaya wamekuwa wakitumia sheria hiyo vibaya kutokana na kushindwa kuielewa vema ambapo aliwataka kabla ya kufanya hivyo kuomba ushauri kwake ambapo atawapa muongozo.

“Sitafurahishwa na wakuu wa wilaya watakao tumia sheria namba 19 ya tawala la mikoa na na mitaaa ambayo inatoa uwezo kwa Mkuu wa wilaya kumuweka mtu kizuizini kwa masaa 48 iwapo mtu akishukiwa kuwa ni muhalifu au anayehatarisha utulivu na amani, sheria hii muiangalie sana…baadhi ya wakuu wa wilaya wamekuwa wakitumia vibaya,” amesema Kagaigai.

Mbali na hilo amewaagiza kuhakikisha wanasiamia ukusanyaji wa mapato ya halmashauri sambamba na kuthibiti mianya ya wizi na ubadhifu wa fedha za serikali kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.

“Mkasimamie mapato ya Fedha za serikali katika halmashauri zenu,mkadhibiti wizi na ubadhirifu wa fedha za serikali na mkayafanye haya kwa kuzingatia sheria. Msisahau pia kuacha milango yenu wazi kwaajili ya kutatua kero na changamoto zinazo wakabili wananchi,” amesema Kagaigai.

Akizungumza wakati wa zoezi la kuapishwa kwa wakuu wa wilaya hao, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi, amewataka wakuu hao kuishi kwa kufuata maadili ikiwa ni pamoja na kufungua milango kwa ajili ya kuwatumikia wananchi kwa haki.

“Kuwa DC ni jambo moja na kuuishi ni jambo jingine msifunge milango yenu, kawatumikieni wananchi kwa haki mkifanya hivyo mtasaidia kuitekeleza ilani ya chama chetu,mkitaka kuleta fujo mtaleta na mkitaka kuketa maendeleo mtaleta tunawategemea,” amemsema Boisafi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles