26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

RC Makalla ataka mikakati mipya Machinga Complex

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, amewaelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuja na Mpango Mkakati wa kuendeleza na kukuza soko la Machinga Complex.

Amesema lengo la kufanya hivyo ilikuwa ni kuweza kusaidia soko hilo liwe kimbilio kwa machinga na wateja.

Makalla ametoa maelekezo hayo mapema leoJumanne Juni 22, 2021 jijini Dar es Salaam, alipotembelea soko hilo na kusikiliza kero za wafanyabiashara, ambapo wamemueleza sababu zinazopelekea wafanyabiashara kulikimbia soko hilo na kwenda mitaani.

Miongoni mwa kero zilizotolewa na wafanyabiashara hao ni mazingira mabovu ya kufanya biashara, utaratibu mbovu wa kupata vizimba, kodi kubwa, sheria kandamizi, ushirikiano mbovu wa viongozi, umeme, maji, vyoo, maji taka, miundombinu isiyorafiki na utaratibu wa kulipa kodi ya mwezi badala ya ushuru wa siku.

Kutokana na malalamiko hayo, Makalla amewaelekeza Mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa Jiji kuhitisha vikao vya mara kwa mara na Wafanyabiashara hao na kupeana mrejesho wa utatuzi wa kero zao ili mwisho wa siku biashara zifanyike na Serikali ipate Mapato.

Aidha, Makalla ameelekeza viongozi wa soko hilo kuachana na tabia ya kufungia biashara za wapangaji wanaoshindwa kulipa Kodi na badala yake wakae mezani kuangalia namna bora.

Pamoja na hayo Makalla ameelekeza Halmashauri ya Jiji kufuatilia fedha za NSSF zilizotolewa Kama mkopo wa Ujenzi wa jengo hilo lili kujua Kama mkopo umemalizika au bado deni lipo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles