25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Abadilika rangi mwilini na kuwa bluu

Mwandishi Wetu

Mwaka 2008, Dunia ilikutana na Paul Karason, mwanamume aliyegeuka kuwa wa rangi ya bluu ku­tokana na kuzidisha dozi ya dawa aliyoinywa na kuipaka katika ngozi yake iliyolenga kutibu madoa madoa usoni.

Miaka mitano baadaye, mtu huyo aliyekuwa gumzo mitandaoni baada ya kuchomoza mbele ya dunia na katika ulimwengu wa tiba, ambao ulianza kufanya tafiti kile kilichomsumbua na hatimaye kubadilika rangi ya ngozi yake akafariki dunia.

Karason alizaliwa akiwa na ngozi ya kawaida, lakini pia mvulana mwenye madoa doa usoni akiwa na nywele zenye mchanganyiko wa wekundu na kahawia.

Lakini baadaye akapata ngozi ya bluu kabla ya mshtuko na nywele zake nazo kugeukia weupe, ikiwa ni ma­tokeo ya maradhi ya nadra yanayoitwa argyria.

Argyria au argyrosis ni hali inayo­sababishwa na wingi wa madini ya kemikali za fedha au vumbi la madini hayo. Dalili kubwa zaidi ya argyria ni kwamba ngozi hugeuka kuwa bluu, au zambarau au zambarau-kijivu.

Katika kujaribu na kukabili maradhi ya ngozi yake usoni, Karason pia alianza kutumia dozi za ‘colloidal silver, ambazo ni za kimininika cha rangi ya fedha.

Karason alikuwa na umri wa miaka 62 wakati alipofariki dunia Septemba 2013 katika Hospitali ya Washington, nchini Marekani, ambako alilazwa baada ya kuugua shambulio la moyo na baadaye kupata maradhi ya pneumonia na kiharusi kikali, hii ni kwa mujibu wa mkewe Anna Karason

Rangi ya ngozi yake ilimpatia umaarufu kiasi cha kuitwa ‘Papa Smurf,’ neno ambalo, mjane wake anasema alilifurahia tu wakati lilipo­toka midomoni mwa watoto.

Jina hilo la utani lililomaanisha kikaragosi mtu maarufu katika tel­evisheni cha rangi ya bluu, alilikubali kutegemeana na nani aliyelisema.

Kwa mfano, iwapo ni mtoto aliyem­kimbilia akisema ‘Papa Smurf,’ utaona tabasamu likipamba katika uso wake, lakini iwapo linatoka mdomoni mwa mtu mzima, huwa hafurahii.

Karason alivuma katika mitandao ya jamii kwa miaka kadhaa kwa kuwa na ngozi hiyo bluu chakavu kufuatia matumizi ya dozi kwa zaidi ya mwongo mmoja zilizolenga kutibu maradhi ya ngozi usoni mwake.

Aliishi maisha ya kujitenga sana hadi alipojitokeza katika vipindi vya televisheni mwaa 2008 akianzia NBC kujadili hali yake hiyo inayojulikana kwa kitaalamu kama argyria.

Karason alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 62 baada ya kutibiwa maradhi ya pneumonia katika hospitali ya Washington baada ya kuugua sham­bulio la moyo. Awali pia alikumbwa na kiharusi kikali,.

Aidha, Mtandao wa Habari wa ABCNews ulimfanyia mahojiano Kara­son mwaka huo, wakati akiishi Oregon. Katika mahojiano hayo, alisema rangi yake ya ngozi bluu ilianza mwongo mmoja uliopita kabla ya hilo aliona tangazo katika jarida moja likiipigia chapuo ‘colloidal silver.’

Aakaondokea kuitumia sana kwa siku akiitengeneza mwenyewe nyumbani na hakuwa amebaini wakati mabadiliko ya ngozi yakijitokeza, hadi rafikiye wa zamani alipomtembelea na kumshtua.

“Na aliniangalia na kusema, Ume­fanya nini usoni?’ ‘sina chochote usoni mwangu!” Karason alimjibu.

Anasema: “Sawa, inaonekana umepaka kitu kama vipodozi au kitu fulani zambarau. Akaendelea kusema kwamba ile ngozi yangu ya awali haipo tena badala yake ana mwonekano mpya na hapo ndipo akashtuka.

Wakati katika miezi hiyo ya awali, akiwa hajaona dalili ya mabadiliko ya ngozi yake bali aliyashuhudia katika afya yake.

“Nilianza kuhisi baridi yabisi katika mabega yangu, hali ilikuwa mbaya, sikuweza kuvua fulana. Na kitu kilichofuata, baadaye hali ikatoweka mithiri ya homa ya vipindi,” anasema. Na iwapo aliamini colloidal silver ingemponya, Karason alisema, “Si­kuwa na shaka na hilo katika moyo wangu”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles