Na BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM.Â
MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imetoa mafunzo juu ya maboresho mapya ya mfumo wa ritani ”return” za kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa walipa kodi wa mkoa wa Kinondoni ili kuwawezesha kupata kuelewa wa mfumo huo kabla ya kuanza kulipa kodi.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mafunzo hayo, Kaimu Meneja Usajili na Uwasilishaji Ritani wa (TRA) Hamidu Athumani amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu ambapo kwa sasa wameanza na wafanyabishara 500 katika wilaya kinondoni.
Alisema wanatoa mafunzo hayo kwa walipa kodi kwa kuwa, Ritani ya VAT imefanyiwa maboresho mbalimbali ikiwemo eneo la ujazaji na viambatanisho vyake hivyo ni vema wakatoa mafunzo hayo kwa wafanyabishara waliosajiliwa na VAT ili wajue namna ya ujazaji wa marekebesho katika Ritani kabla ha mfumo wenyewe kuanza kufanya kazi.
Aliongeza kuwa, kwa kupitia mfumo huo mfanyabiashara ataweza kufanya marekebisho mwenyewe ya Ritani za VAT bila ya kuandika barua kama awali ambapo huku pia maboresho makubwa yakiwa yamefanywa katika eneo la kuweka risiti za kietroniki ambazo zinakuwa hazijajazwa .
“Zamani mtu alikuwa anaweza kujaza Ritani na kuweka risiti hata kama ameiokota lakini baada ya Maboresho haya mtu hataweza kujaza Ritani katika risiti isiyokuwa ya Kwake,” alisema.
Aidha Hamidu alisema, mafunzO hayo ni endelevu na wamejipanga kuwafikia Wafanyabiashara nchi nzima ambapo kwa kuanzia wameanza na Mkoa wa Kinondoni.
Na baadae wataenda Kariakao, Ilala na Temeke hivyo wanatarajia ushirikiano mkubwa na wafanyabiashara ili waweze kulipa kinachostahili na serikali iweze kukusanya kinachostahili.
Kwa upande wake, Mfanyabiashara Daniel Lema , alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuondokana na usumbufu wa kwenda kwa Meneja mara kwa mara kujua thamani ya kodi inayodaiwa na badala yake utawarahisishia kufanya biashara zao na kulipa malipo k