26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

JPM: Nataka Arusha iwe kama Calfornia

Nora Damian -Arusha

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli ameahidi mambo manane kwa Mkoa wa Arusha na kusema ana- taka iwe ndiyo Calfornia ya Tanzania.

Jana Dk. Magufuli aliingia mkoani Arusha ukiwa ni mkoa wa 18 kufanya kampeni tangu alipozindua Agosti 29 mwaka huu jijini Dodoma.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, alisema ana mawazo mazuri na Arusha na anataka alibadilishe liwe jiji la kisasa.

Aliyataja mambo ambayo atayaimarisha ni pamoja na biashara ya utalii, madini, ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Aru- sha, biashara ya maua, mbogamboga na matunda, ujenzi wa stendi ya kisa- sa, ujenzi wa barabara, usafiri wa treni ya Dar es Salaam – Tanga – Kilimanjaro – Arusha pamoja na kuimarisha hu- duma za elimu, afya, maji na umeme.

“Arusha ni mji wa watu wanao- jishughulisha wanapenda maendeleo, tunataka kutengeneza mabilionea ndani ya Arusha na ndani ya Tanzania, utalii upo, Tanzanite ipo, madini men- gine yapo kwanini tushindwe kwenda mbele…Arusha jiji litapaa.

“Nina mawazo mazuri na Arusha nataka iwe ndiyo Calfornia ya Tanza- nia na hili halishindikani,” alisema Dk. Magufuli.

Dk. Magufuli aliahidi kukamilisha ujenzi wa barabara ya Mto wa mbu – Loliondo kilomita 164 ambayo alisema ilianza kuombwa tangu enzi za Lo- wasa, kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa kilomita 430, Longodo – Sanya juu kilo- mita 65 na Arusha – Kigongo kilomita 8.8.

Kuhusu afya alisema katika kip- indi cha miaka mitano ijayo watajenga hospitali, vituo vya afya, zahanati, kuongeza watumishi na bajeti ya dawa na vifaa tiba na kuahidi kuwa watajenga jengo la huduma ya uchunguzi la daraja la kwanza.

Akizungumzia mradi wa maji wenye thamani ya Sh bilioni 520 Dk. Magufuli alimtaka mkandarasi kuharakisha ili ifikapo Desemba wananchi wa Wilaya za Arumeru, Simanjiro na Hai waanze kupata maji.

Kwa mujibu wa Dk. Magufuli mradi huo unatarajiwa kuzalisha lita milioni 160 wakati mahitaji ya maji katika Jiji la Arusha ni lita milioni 106 na yanayozalishwa sasa ni lita milioni 40 hivyo kuwa na ziada ya lita milioni 100.

“Haiwezekani watalii wanatoka Ulaya wanafika hapa wanakosa maji, nitakapochaguliwa tutakwenda ku- malizia huu mradi ili suala la maji liwe historia,” alisema Dk. Magufuli.

Kwa upande wa umeme alisema mpaka sasa vijiji 256 vina umeme na kuahidi 136 vilivyobaki vitapata umeme ndani ya miaka miwili.

“Kwa nchi nzima hivi sasa tumefikia asilimia 85, miaka mitano ijayo suala la umeme vijiji vyote Tanzania tutalimaliza,” alisema.

Kuhusu mkakati wa kuimarisha usafiri wa reli alisema watanunua ma- behewa 800 ya mizigo, 37 ya abiria na vichwa 37 iki kurahisisha usafirishaji wa mizigo na kuwapunguzia gharama wafanyabiashara.

“Tunataka tutengeneze mazingira ya watu kuwa matajiri, tumefufua usafiri wa reli ambao haukuwepo kwa zaidi ya miaka 30, nataka hii treni muitumie kutengeneza pesa itapunguza gharama za usafiri wa mizigo… tutakuwa na treni zenye ‘cold facilities’ ziweze kusafirisha bidhaa za mboga na nyingine,” alisema Dk. Magufuli.

Aidha alisema atapanua bandari ya Tanga ili mafuta na mizigo mingine iwe inateremshiwa Tanga bei ya mafuta ishuke chini.

Alisema pia ataendeleza sekta za kilimo, mifugo na viwanda kwani zin- achangia kutoa ajira na kukuza mapato ya wananchi na nchi kwa ujumla.

“Sekta ya kilimo kwa hapa Arusha inachangia asilimia 26.5 ya pato la mkoa lakini kwenye ngano hatujafanya vizuri sana, Tanzania inaagiza tani 800,000 zaidi ya Sh trilioni 1.3. Ninawaomba wana Arusha, Manyara na mikoa ya jirani tusimamie vizuri na zao la shairi ili Serikali isiendelee kuagiza ngano toka nje,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Magufuli bi- ashara ya matunda, mbogamboga na viungo imetoa ajira milioni 4 na kuongeza mauzo kutoka Dola milioni 412 hadi Dola milioni 779.

Pia aliahidi kutoa ruzuku kwa mabwawa ya wafugaji, kuchimba mabwawa na kujenga machinjio.

Alisema akichaguliwa tena ataimarisha biashara ya utalii ili wananchi waendelee kufaudika kwa sababu Arusha ni kitovu cha utalii kwani asilimia 80 ya watalii hupitia katika mkoa huo.

Dk. Magufuli pia alimuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kushughulikia malalamiko ya wa- nanchi dhidi ya askari polisi wanaodaiwa kuwaomba rushwa wananchi wakati wa kuomba dhamana.

KUHUSU GAMBO

Katika mkutano huo Dk. Magufuli aliwataka wananchi kupuuza propa- ganda chafu na kwamba hamchukii mgombea ubunge Arusha Mjini, Mrisho Gambo na wala hakumfuku- za.

Alisema alitengua uteuzi wa Gambo na aliyekuwa mkuu wa wilaya pamoja na viongozi wengine ambao walimuomba kwa ajili ya kwenda kushiriki katika uchaguzi mkuu.

“Sikumfukuza ukuu wa mkoa wala aliyekuwa mkuu wa wilaya ya hapa alienda kugombea ubunge Ba- bati Vijijini, sasa usingeweza ukawa na RC wakati huo huo anakwenda kugombea ubunge, Chama Cha Mapinduzi kinapenda haki.

“Ndiyo maana wakuu wa mikoa, wilaya, madas waliokwenda ku- gombea nilitengua uteuzi wao na ndivyo nilivyofanya kwa Gambo. Ninashangaa watu wanaposimama kwenye majukwaa wanasema Gambo simpendi, ningekuwa simpendi ningemrudisha jina lake…kama mnataka maendeleo ya kweli mleteni Gambo,” alisema Dk. Magufuli.

Alisema baada ya uchaguzi wa 2015 alipata shida kutokana na Jimbo la Arusha Mjini na kata 24 kuwa chini ya upinzani hali iliyomlazimu kuteua viongozi wa kumsaidia kuharakisha maendeleo akiwamo Gambo na kumsifu kuwa alifanya kazi nzuri.

“Mlinipa kura lakini mkanichagulia wabunge na madiwani ambao hawakutokana na chama changu, nilipata msalaba mkubwa, nilipata shida kupata ‘connection’ ilibidi nianze kutafuta viongozi ambao watanisaidia kuyapeleka yale ninayotaka…mheshimiwa Gambo nakushukuru kwa kazi nzuri sana uliyoifanya hapa Arusha,” alisema.

LOWASA, KINANA

Naye Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa, aliwaomba Watanzania kumpa Dk. Magufuli zawadi ya kura nyingi kutokana na kazi nzuri aliyoifanya katija uongozi wake.

“Leo Venezuela, Angola kuna fujo kwa sababu ya mambo ambayo sisi yanatuletea amani, rais Magufuli amekuja na ndoto sahihi alihakikisha corona haiji kwetu, anajitahidi na wananchi wanamwelewa…sasa tumpe zawadi ya kura,” alisema Lowasa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abudulrahman Kinana, alisema Dk. Magufuli anastahili kuchaguliwa tena kwa sababu ametekeleza ilani, ametekeleza ahadi alizotoa wakati anafanya ziara mikoani na ahadi mpya alizonazo kwa miaka mitano ijayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles