24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kunenge afika Mbezi Luis kushuhudia kontena zilizokuwa zimekwama bandarini

Brighiter Masaki

Kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Abubakar Kunenge kuitaka taasisi ya TICTS kuhakikisha kontena sita zenye Vifaa vya Ujenzi wa Stand mpya ya Mbezi Luis zilizokuwa zimekwama Bandarini kutoka ndani ya masaa mawili, hatimae Taasisi hiyo imetekeleza mara moja agizo hilo.

Mapema leo Kunenge amefika Stand mpya ya Mbezi Luis kujihakikishia Kama kontena hizo zimefika ambapo amethibitisha kujionea kontena zote sita zimefika na kufanya idadi kontena zilizotoka kufikia 14.

Aidha Kunenge amebainisha kuwa kontena zilizofika ndani yake Kuna Vifaa mbalimbali vikiwemo Vioo, Fremu za madirisha, Mabati na kueleza kuwa Vifaa hivyo vimeanza kutumika Mara tu vilipofika.

Hata hivyo Kunenge ameendelea kumtaka Mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili Stendi hiyo ikamilike kabla ya November 30 Kama alivyoagiza Rais Dkt. John Magufuli wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi.

Itakumbukwa siku ya Jana October 23 RC Kunenge alifanya ziara ya kustukiza kwenye Bandari ya Dar es salaam kufuatilia kinachokwamisha kutoka kwa kontena hizo na kubaini kasoro za kiutendaji na kuamua kutoa maagizo ya kutaka kontena hizo zitoke ndani ya masaa mawili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles