25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Barrick yasisitiza kuilipa Tanzania Sh bil 700

Mwandishi -Dar es salaam

SIKU chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kupokea gawio la zaidi ya Sh bilioni 100 kutoka Kampuni ya Madini ya Twiga inayomilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick, kampuni hiyo imesisitiza kuilipa Serikali Sh bilioni 700ambazo zitatolewa kwa nia ya kumaliza mzozo uliokuwepo kati yake na Acacia.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.

Katika taarifa hiyo alisema mbali na malipo ya kwanza ya Dola za Kimarekani milioni 100, Barrick imeweza kulipa mirahaba na ushuru wa Dola za Kimarekani milioni 200 kwa serikali.

“Na wiki iliyopita kampuni yaTwiga kwa mara ya kwanza ilitoa Dola za Kimarekani milioni 250, hivyo kwa mujibu wa makubaliano baada ya Barrick kuchukua shughuli za iliyokuwa kampuni ya madini ya Acacia tutailipa Serikali ya Tanzania Dola za Kimarekani milioni 300 (takribani shilingi bilioni 7000).

“Ukweli ni kwamba mambo mengi yameweza kufanikiwa ndani ya muda mfupi na ni dhihirisho ya ninachokiamini ushirikiano wa kwanza na wa aina yake Afrika.

“Huku makubaliano ya mfumo sasa yakiwa yametekelezwa kikamilifu, tumesuluhisha mizozo mingi ya wa miliki wa ardhi na tuko katika hatua nzuri kuhakikisha mizozo mingi ya wamiliki wa ardhi inamalizika na tutahakikisha tunatii kikamilifu vibali vyetu vya mazingira ikiwemo sheria za serikali,”alisema Bristow.

Vilevile katika taarifa hiyo, Bristow alisema ukarabati wa mgodi wa North Mara uko mbioni kukamilika tofauti na muda uliopangwa.

“Na Bulyanhulu imeanza tena shughuli za uchimbaji wa chini ya ardhi na imepangwa kuanza usindikaji wa madini ya chini ya ardhi mwishoni mwa mwaka huu.

“Tunakusudia kuifanya North Mara na Bulyanhulu kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha kuwa inakuwa migodi ya kiwango cha kwanza kwa uzalishaji inayoweza kutoa angalau dhahabu ounces 500,000 kila mwaka,”alisema.

Aidha, katika hatua nyingine alifafanua kuwa, Barrick imetunukiwa tena leseni 10 mpya za uchimbaji hapa nchini na imepanga kutumia dola milioni nane kuchimba maeneo hayo kwa mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles