26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

HRW: Jeshi DRC linaunga mkono jinai za waasi

BRUSSELS, UBELGIJI

SHIRIKA la Human Rights Watch limesema katika ripoti yake mpya kuwa, wapiganaji watiifu kwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wanaendelea kufanya mauaji, kubaka na kuajiri watoto kwa lazima kwa kuungwa mkono na jeshi la nchi hiyo.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa wapiganaji wa Guidon Shimiray Mwissa, wanaendelea kutenda jinai dhidi ya raia kwa kusaidiwa na jeshi. 

DRC mwezi Juni mwaka jana ilitoa waranti wa kumtia mbaroni Guidon Shimiray Mwissa kwa kushiriki katika uasi, kuwaajiri watoto kuwa askari na kutekeleza vitendo vya ubakaji mashariki mwa nchi. 

Guidon aliye na umri wa miaka 40 ni kutoka katika kabila la Nyanga na mwanajeshi wa zamani wa serikali kutoka Mkoa wa Walikale ambaye aliasi jeshi mwaka 2007 na kuwa mpiganaji muasi.

Muda mfupi baadaye, Shimiray alijiunga na Harakati ya Nduma Defence of Congo (NDC) chini ya uongozi wa Ntabo Ntaber Sheka. 

Aidha mwaka 2014 alijitenga na Sheka na kuasisi harakati kwa jina la NDC-R. 

Thomas Fessy, Mtafiti wa ngazi ya juu wa Shirika la Human Rights Watch alisema, waranti uliotolewa mwaka 2019 kwa ajili ya kumtia mbaroni kiongozi huyo wa waasi haukumzuia kutenda jinai za kutisha dhidi ya raia wa Kongo katika maeneo aliyokuwa akiyadhibiti. 

Alisema waungaji mkono wake ndani ya jeshi la Kongo wanapasa kuchunguzwa na kushtakiwa kwa kosa la kutumia kundi la jinai kama wakala wa usaidizi.

AFP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles