26.3 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yampiga changa la macho Hemed Morocco

HEMED moroccoNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

KATIKA hali isiyotarajiwa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imempa mkataba ‘feki’ Mkurugenzi wake mpya wa ufundi, Hemed Morocco, badala ya ule waliokubaliana awali.

Kwa mujibu wa Morocco, mkataba aliopewa jana ulikuwa na upungufu katika kipengele cha malipo, tofauti na kiwango walichokubaliana.

Morocco aliliambia MTANZANIA kuwa bado kuna sintofahamu katika makabuliano yake na uongozi wa klabu ya Simba ili kutua Msimbazi.

“Kila kitu kimeenda sawa kama tulivyoongea Zanzibar kabla ya kuonyeshwa mkataba, lakini kipengele kimoja cha malipo kimeleta sintofahamu.

“Nimewaletea mahitaji yangu nasubiri na wao waniletee yao tuone, lakini bado tunaendelea na mazungumzo kwani wameniomba niwape muda wa kufikiria hivyo nasubiri maamuzi yao,” alisema Morocco ambaye pia ni kocha msaidizi wa Taifa Stars.

Alisema yupo tayari kukinoa kikosi hicho kama dili hilo litatiki na mahitaji yake yatasikilizwa kama anavyotaka.

Hata hivyo, hali hiyo ya klabu hiyo kongwe kukiuka makubaliano na Morocco, imezua minong’ono kwa wadau wa soka nchini hususan kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Wadau wameonekana kuilaumu klabu hiyo kuwa inataka kuyarudia yale ambayo imekua ikiyafanya kwa wachezaji wake huku wakikumbushia mgogoro wa kimkataba kati ya klabu hiyo na aliyekuwa mchezaji wa Simba, Ramadhan Singano ambaye alihamia Azam.

Hawakuishia hapo, walikumbushia mgogoro wa Athuman Idd ‘Chuji’, hata ule wa Kelvin Yondan na klabu hiyo, ambao viongozi wa Simba walituhumiwa kufoji sahihi kwenye mikataba ya wachezaji hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles