28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

SIMBA YAVAMIA MBEYA

 MOHAMED KASSARA -DAR ES SALAAM 

KIKOSI cha Simba kilitua jana mkoani Mbeya kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ihefu, utakaochezwa Jumapili hii Uwanja wa Sokoine jijini humo. 

Msafara wa kikosi hicho ulitokea mkoani Arusha, ambako Simba ilicheza na Namungo mchezo wa Ngao ya Jamii, uliopigwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na Wekundu hao kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. 

Baada ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa tatu mfululizo, juzi kikosi cha Simba kilijipima nguvu dhidi ya Arusha FC na kuvuna ushindi wa mabao 6-0.Kikosi hicho kilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam asubuhi kikitokea Arusha kabla ya kuunganisha kwa usafriki wa ndege kwenda Mbeya, tayari kwa kuikabili Ihefu iliyopanda Ligi Kuu Bara msimu uliopita. 

Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja wa kikosi hicho, Patrick Rweyemamu, alisema wameamua kutua mapema Mbeya wakilenga kuzoea hali ya hewa ya baridi iliyopo mkoani humo kipindi hiki. 

Alisema kuwa wanataka kuhakikisha wanaanza vema kampeni zao za kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya nne mfululizo. 

 “Tunashukuru tumefika salama, kikosi kipo kamili, kila mchezaji ana morali, tumekuja mapema ili kuzoea mazingira, tunajua hali ya hewa ya mbeya ni tofauti na Dar es Salaam, hata wapinzani tunaokutana nao si wakubeza. 

“Tumecheza michezo kadhaa ya kirafiki, kocha ameona kikosi chake kilivyo, tumeufungua vizuri msimu kwa kushinda Ngao ya Jamii, tunataka kuendeleza hilo hadi mwisho wa msimu, tunajua msimu huu ligi itakuwa ngumu, lakini sisi kama mabingwa watetezi tumejipanga vilivyo kupigania taji letu,”alisema Rweyemamu. 

Simba imecheza michezo minne ya kirafiki ikiwemo dhidi ya Vital’O ya Burundi katika kilele cha siku ya Simba Day na kuibuka na ushindi wa mabao 6-0, ikaifumua KMC mabao 3-1, ikaitungua Transit Camp mabao 5-2 kabla  ya kuibomoa AFC mabao 6-0. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles