29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yatoa mikopo ya Sh bilioni 63.4 halmashauri

Nathaniel Limu-Singida 

SERIKALI kupitia halmashauri za wilaya, manispaa na majiji nchini, imetoa mikopo ya zaidi ya Sh bilioni  63.4 zenye mashariti nafuu kwa wanawake wajasiriamali, kati ya mwaka 2015 hadi sasa.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto,Dk. John Jingu alisema lengo la mikopo ni kuinua kipato cha familia na kukuza ustawi wa kaya.

Hotuba hiyo ya katibu mkuu iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu, Patrick Golwike ilikuwa ya uzinduzi wa kongamano la kiuchumi la wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Singida jana.

Alisema Serikali kupitia utengaji wa asilimia nne ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya wanawake,jumla ya wanawake wajasiriamali 938,802 wamenufaika na mikopo hiyo.

“Mikopo hii yenye masharti nafuu,imewajengea ujasiri wanawake,kukuza ujuzi na mbinu za ujasiriamali. Pia wanawake hao wameweza kujiunga na mitandao ya masoko mbalimbali.Kwa njia hiyo wamekuwa na uwezo wa kuchangia pato la taifa.

“Wizara inafanya kazi na baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi kuhakikisha majukwaa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, yameanzishwa kila mkoa kwa sababu washiriki walio wengi ni wanawake,”alisema.

Alisema ni matarajio  majukwaa ya wanawake yaliyoanzishwa kila mkoa,yatakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi.

“Kupitia majukwaa haya, wanawake watabadilishana uzoefu wa uzalishaji mali. Kingine ni upatikanaji wa masoko ya bidhaa wanazozalisha, matumizi ya teknolojia rahisi za uzalishaji mali”,alisema.

Naibu Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Beatus Choaji alisema mafanikio ya Tanzania kufikia uchumi wa kati, kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na anawake

Alisema kazi iliyopo  sasa ni kuhamasisha na kuelimisha wanawake kutambua fursa  mbalimbali za kiuchumi zilizopo,  na mbinu bora za kutafuta  masoko.

Mwakilishi wa Mkurungenzi wa Maendeleo ya Jinsia, Sylvia Siriwa aliwahimiza wanawake wa mkoa huo kujipanga mapema ili waweze kunufaika kiuchumi, kupitia miradi mikubwa inayotarajiwa kupitia mkoani humo.

“Mkoa wa Singida una bahati ya kupitiwa na  bomba la mafuta linaloanzia Uganda  hadi Tanga.Mkoa huo utapitiwa na ujenzi wa reli ya kisasa ya mwendokasi. Kazi iliyopo mbele yenu sasa ni kujiandaa.. 

Alisema sasa kasi ya ongezeko la  wakazi wa Jiji la Dodoma ni kubwa mno.

“Muda si mrefu mkoa wa Dodoma utashindwa kujilisha, kuwahudumia wakazi wake. Kwa hiyo ninyi wanawake wajasiriamali na wakazi wengine wa mkoa wa Singida,jiandaeni na fursa hii ya kuwa jirani na makao makuu ya nchi,”alisema. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles