24.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru yaokoa Sh milioni 41

Na Walter Mguluchuma- Katavi

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Katavi wamefanikiwa kuokoa na kurejesha Sh milioni 41.117 ikiwamo zaidi ya Sh miloni 23 zilizokuwa zimeibiwa kutoka na  kugushi safari hewa na mikutano hewa. 

 Taarifa ya kuolewa fedha hizo ilitolewa jana na Mkuu wa Takukuru wa Mkoa wa Katavi, Cristophar Nakua alipokuwa akizungumza ofisini kwake jana mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera.

Alisema Takukuru Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Takukuru Wilaya ya Tanganyika, wameokoa fedha hizo ambazo zilikuwa zimeibiwa.

Alisema Sh milioni 15 ni mali ya Shule ya Msingi Kamjela  katika Wilaya ya Tanganyika ambazo zilikuwa zimelipwa  kwa mkandarasi Sayi Busines wa Mpanda  aliyekuwa  akifanya  kazi ya kusambaza vifaa vya ujenzi katika Shule ya Msingi Kamjela fedha ambazo  zililipwa na  kuchukuliwa isivyo halali toka Benki ya NMB  Mpanda.

 Nakua alieleza kuwa kutokana na kazi aliyofanya   mkandarasi huyo alikuwa amelipwa kwa hatua anayostahili lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida  Takukuru kupitia Wilaya ya Tanganyika iligundua Sh  15 zilitolewa kinyuma cha utaratibu .

Alisema uchunguzi wa Takukuru ulifanyika na kufanikiwa kuwakamata na kuwahoji watuhumiwa na waliweza  kufanikiwa kuziokoa na kurejesha fedha hizo  ambazo  zimekabidhiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tanganyika, John Romuli ili azirejeshe  katika Shule ya Msingi Kamjela.

 Alisema fedha nyingine Sh milioni 23 .045 ambazo zilikuwa zimeibiwa na baadhi ya watumishi wa umma  kwa kugushi safari hewa na posho hewa  za vikao.

Alisema fedha hizo zitaingizwa kwenye mfuko Mkuu wa Serikali kupitia akaunti ya Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ili ziweze  kufanya shughuli nyingine za Serikali .

Alisema pia Sh milioni 1.8 zilizokuwa zimekusanywa kama mapato ya Serikali kwa mfumo Point Of Sale (POS)  ambazo zilikuwa zimeibiwa na hazikuwasilishwa serikalini  kama utaratibu  unavyotakiwa  zimerudishwa Serikalini  ili ziweze kutumika ilivykusudiwa.

Mkuu huyo wa Takukuru alisema Sh milioni 1.7 zilizorejeshwa kutokana na operesheni waliofanya ya kufatilia wadaiwa sugu wa SACCOS ya  walimu ya Mpate   SACCOS, wamezikabidhi kwa viongozi  wa chama  hicho  ili wawze  kuwalipa  wanachama wanaoidai.

 Kwa upande wake  Homera alisema aliwapongeza Takukuru akisema wamekuwa  wakifanya kazi zao vizuri  na kwa uadilifu kubwa .

 Aliwataka  wafanye utaratibu wa kuzifanyia ukaguzi SACCOS  zote zilizopo katika Mkoa wa Katavi kwani zinachangamoto kubwa ya ubadhirifu wa fedha.

 Homera aliwasisitiza wakurungezi wa halmashauri zote za mkoa huo kuwa makini kila wanapokuwa wanaizinisha malipo ili waweze kubaini na mapema ubadilifu wowote ambao unaweza kutokea kwenye halmashauri zao.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, John Romuli, alisema Takukuru wamekuwa wakifanya kazi kubwa hivyo wanaiomba  kwenye baadhi ya maeneo  wanahitaji ushirikiano wa kutoka kwenye Taasisi hiyo .

Alisema asilimia 10 ya mapato ya halmashauri ambazo zizotolewa kwa makundi ya wanawake, vijana na wazee zimekuwa hazirudishwi pamoja na jitihada zinazokuwa zinafanywa na halmashauri hivyo wanaomba ushirikiano wa Takukuru kuwasaidia watu wazirejeshe fedha hizo .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles