28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wagombea ubunge CCM waanza kuchukua fomu za NEC kila kona

NA UPENDO MOSHA -KILIMANJARO

SIKU moja baada ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutoa majina ya wagombea walioteuliwa kuwania ubunge kupitia chama hicho, jana baadhi wamejitokeza kuchukuoa fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) za kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo.

Mkoani Kilimanjaro, waliochukua fomu hizo ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei, anayegombe Jimbo la Vunjo, Prof Adolfu Mkenda, Jimbo la Rombo, Profesa Patrick Ndakidemi Moshi vijiji, Priscus Tarimo, Moshi Mjini, Saashisha Masue, Jimbo la Hai, Joseph Thadayo, Jimbo la Mwanga, Anna Kilango, Same Mashariki na Mathayo Devid Jimbo la Same Magharibi.

Wagombea hao kwa nyakati tofauti walijitokeza katika ofisi za halmashauri kuchukua fomu hizo kwa lengo la kupewa ridhaa ya kupeperusha bendera za chama hicho tawala katika nafasi ya ubunge.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kuchukua fomu hizo, wagombea hao walisema wameamua kuomba nafasi ya ubunge kutokana na dhamira za kweli zilizopo ndani yao katika kuwatumikia wananchi katika maeneo yao.

Saashisha Mafue ambaye ni mgombe wa ubunge Jimbo la Hai (CCM), alisema amechukua fomu na kwamba kinachofuata ni kufuata maelekezo yote yaliyotolewa na chama bila kukiuka kanuni zozote za uchaguzi.

“Hii nayo ni hatu, namshukuru Mungu, chama changu na wajumbe ikiwemo viongozi wangu, leo sina mengi zaidi nataka mtambue ninayo kiu ya dhati kuwafanyia wananchi maendeleo katika jimbo langu”alisema

Naye Joseph Tadayo ambaye ni Mgombea Ubunge Jimbo Mwanga, alisema alianza mchakato wa kuomba ridhaa ya kugombea kwa miaka mingi na kwamba sasa anakishukuru chama hicho kwa kumuamini na kupewa ridhaa ya kugombea ubunge na kuwataka wananchi kuwa watulivu kusubiri kipenga cha uchaguzi kupulizwa rasmi ambapo atamwaga sera zake zote hadharani.

Awali Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabhiya, aliwataka wagombea wote kuwa watulivu ikiwemo kuzingatia maelekezo, kanuni na sheria zote za uchaguzi ili kukithi matatakwa ya tume.

“Wagombea ubunge kwa siku ya leo (jana) wamechukua fomu katika majimbo yote nane isipokuwa Jimbo la Siha,  kazi hii uliyoifanya itakuwa njema sana kama wataheshimu kanuni zote za tume ya uchaguzi maana CCM imerudisha majembe hatuna mashaka watu wetu wanauzika vizuri kwa wananchi”alisema

Dar/Pwani

Katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, pia baadhi ya walioteuliwa jana walijitokeza kuchukua fomu za NEC za kuomba kuteuliwa kuviwakilisha chama chao kwenye kinyang’anyiro hicho.

Katika jimbo la Ubungo jijini Dar es salaam, jana saa 4 asubuhi Profesa Kitila Mkumbo alichukua fomu ya kuwania ubunge.

Kitila ambaye alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji aliwasili katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi akiwa amesindikizwa na wanachama wengi.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Kitila alisema atahakikisha anafanyia kazi changamoto zilizopo katika jimbo hilo ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Naye Abas Tarimba anayegombea Jimbo la Kinondoni,  kwenye ofisi za msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Kinondoni akiahidi kusukuma miradi ambayo imesimama na kutatua kero nyingine zinazowakabili.

Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega ambaye ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, alichukua fomu akisema  ameamua kuwania tena nafasi hiyo ili aweze kuendelezwa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa tangu Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani.

Wengine waliochukua fomu jana asubuhi ni Silvester Koka anayewania Jimbo la Kibaha na Ridhiwani Kikwete anayeyetea ubunge wa Jimbo la Chalinze Mkoa wa Pwani.

Kikwete kwa upande wake alisema CCM inaingia katika uchaguzi huu ikiwa kifua mbele kwa kuwa katika kipindi cha miaka mitano imeweza kutekeleza miradi mingi ya Maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles