28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Hospitali ya Rufaa Morogoro yakabiliwa uhaba wa damu

Na Ashura Kazinja -Morogoro

HOSPITALI ya Rufaa Mkoa wa Morogoro inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa damu katika Kitengo cha Damu Salama.

Imeelezwa hali hiyo inatokana na watu kutojitolea kutoa damu kwa muda sasa kutokana na Serikali kupiga marufuku mikusanyiko isiyo ya lazima.

Hayo yalisemwa jana na Mratibu wa Kitengo cha Damu Salama Mkoa wa Morogoro, Hashim Ally.

Alisema awali makundi mbalimbali yalikuwa yanajitolea damu mara kwa mara, lakini baada ya kuzuka ugonjwa wa Covid-19,  watu wamekuwa na hofu na kushindwa kujitokeza wakihofia mikusanyiko.

Ally alisema kutokana na hali hiyo, wamelazimika kuomba msaada wa kikundi cha Saydo Kareti ili kuchangia damu.

“Limekuwepo tatizo kubwa la upatikanaji wa damu kipindi hiki, tunapata damu kwa taasisi kama Saydo na Magereza, bado upatikanaji ni mdogo ikilinganishwa na matumizi.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Rita Lyamuya alisema kutokana na hospitali hiyo kuwa tegemezi kwa halmashauri za mkoa huo, inatumia zaidi ya uniti 300 za damu kila mwezi.

Aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kujitolea damu ili kuokoa maisha ya wajazwazito, watoto na majeruhi.

“Kuna uhitaji mkubwa wa damu katika hospitali yetu, wastani tunatumia damu uniti 300 mpaka 430 kwa mwezi, tunachofanya leo (jana) ni cha kusaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wetu,” alisema Dk. Lyamuya.

Kiongozi wa Kikundi cha Saydo Kareti,  Mashaka Salehe alisema licha ya kikundi chao kuhusika na michezo, wanafanya pia shughuli za kusaidia jamii kama usafi na utoaji damu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles