25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Sheikh Chizenga, Prof. Kabudi wamshukuru Magufuli

 CHRISTINA GALUHANGA– DAR ES SALAAM

WAKATI Waislamu wakisherekea sikuku ya Id el Fitr, Katibu wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Hassan Chizenga amempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kutambua silaha namba moja ya kupambana na ugonjwa wa corona ni ibada kwa kumtanguliza Mungu.

Akizungumza katika Msikiti wa Manyema, Dar es Salaam jana, wakati wa swala ya Id EL Fitri, Sheilkh Chizenga.

Chizenga ambaye alimwakilisha Mufti wa Tanzania, Alhaj Abubakar Zuber alisema kitendo cha Rais Dk.Magufuli kuruhusu nyumba za ibada kuendelea kutoa huduma katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona, alikuwa sahihi na kimesaidia mno kupunguza tatizo ambalo linaisumbua duniani.

“Tunamshukuru rais wetu ambaye alitambua umuhimu wa nyumba za ibada na kuruhusu kuendelea kufanyika kwa ibada japokuwa tulipita katika kipindi kigumu, aliruhusu watu waendelee kufanya maombi kila mmoja kwa Imani yake.

“Uamuzi wake, umeipa heshima kubwa Tanzania kimataifa, watu wanajiulize alifanye hadi imekuwa hivi,”alisema. Alisema anamuombea kwa Mwenyenzi Mungu aizidi kumng’arisha, kumtetea, na kumuomgoza katika kipindi cha maisha yake yote.

Katika hatua nyingine, alisema wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakilazimisha kutoa matamko ili mradi jambo fulani lifanyike kitu ambacho si sahihi na endapo linahusu dini ni vema viongozi waliopo ndio wakalizungumzia.

“Baadhi ya watu wamegeuka kuwa wasemaji wa Mwenyenzi Mungu, hii kazi ni ya viongozi wa dini nawashauri Waislamu kuepuka kutoa matamko yoyote ambayo yana athari katika jamii,”alisema.

Katibu wa Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata), Nuhu Mruma alimshukuru Mwenyenzi Mungu kwa kukamilisha funga zao salama na kuomba awapandishe daraja.

Aliwataka Waislamu kuendelea kuyaishi mema na kukamilisha kwa vitendo mazuri yote yaliyokuwa yakifanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan katika kipindi kijacho.

Alisisitiza ni vema kuendelea kuimarisha amani na upendo uliopo hivi sasa hapa nchini ili kujenga Taifa imara na lenye afya bora.

 UCHAGUZI MKUU

Alisema katika uchaguzi mkuu wa viongozi wa kitaifa katika nafasi za udiwani, ubunge na urais, unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu, ni vema wananchi wakatumia fursa yao kikatiba kuchagua au kuchaguana.

Alisema wakati sasa umefika wa kujiepusha kuchagua viongozi kwa sababu ya siasa, udini, ukabila na rushwa ili kupata viongozi bora watakaoongoza kwa misingi bora yenye maendeleo.

Ugonjwa wa Corona

Alitoa pongezi kwa rahisi kutokufungia nyumba za ibada kwani hata maandikio yanasena wakati mgumu ni muhimu kukimbilia maombi na kwenye nyumba hizo.

Alisema jitihada za Serikali na mikakati yake zinasaidia kupunguza idadi ya vifo na mlipuko wa ugonjwa huo.

Alisema wakati huu ambapo kulikuwa na mapambano dhidi ya ugonjwa huo hofu ilikuwa ni kubwa kuliko ugonjwa wenyewe, Serikali imefanyakazi kubwa kuhakikisha wananchi wake wanabaki salama.

“Wakati wowote mgumu ni muhimu kukimbilia kwa Mwenyenzi Mungu tunashukuru Rais Magufuli kwa kuacha nyumba za ibada wazi na maombi etu Mwenyenzi Mungu ameyasikia tofauti na nchi za wenzetu ambao wamepoteza watu wengi kwa ugonjwa huo,”alisema Mruma.

Alisema endapo Serikali ingetangaza zuio la kutoka ndani ‘lockdown’ ingeweza kuleta maafa zaidi katika jamii.

UFUNGUAJI VYUO

Mruma alisema ni wakati sasa kwa wahadhiri, walimu na wakufunzi kufuata tahadhari zote pindi wanafunzi watakaporejea vyuoni na shule.

Alisema jamii nayo inapaswa kubadli tabia na mifumo ya maisha kwa kutenda mema ili Mwenyenzi Mungu awaepushe na mambo mbalimbali.

Alitoa wito kwa viongozi wa kidini na Serikali kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kufuata miongozo mbalimbali iliyowekwa.

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum aliwataka Waislamu kutumia sherehe za Idd kuomba udugu, msamaha na kumpongezana.

Alisema kila mfalme au mtawala ana mipaka yake hivyo katika kusherehekea sikukuu hiyo wasivuke mipaka ya Mwenyenzi Mungu katika kufurahi.

“Tunashukuru Mungu kwa kutuponya na corona mkoa wetu kwa kuwa viongozi wetu walisimamia imara bila kufunga nyumba za ibada, tuliendelea kulia na Mwenyenzi Mungu amesikia kilio chetu,”alisema Salum.

 ZUNGU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Zungu ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika swala hiyo, aliwapongeza Waislamu kwa kumaliza mfungo wa Ramadhan na kuwataka kuendelea kufanya shughuli zao huku wakichukua tahadhali mbalimbali za wataalam wa Afya.

Kwa mwaka huu, Idd imesherehekewa kwa mfumo tofauti na miaka ya nyuma ambapo Bakwata ilizuia kuwapo kwa Idd Kitaifa na Baraza la Idd ili kuzuia mikusanyiko ambayo ingeweza kuchangia maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Kabudi

Katika hatua nyingine, Tanzania imeitaka dunia na jumuiya za kimataifa kutambua kauli ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwahimiza Watanzania kusali na kuliombea taifa kuondokana na maradhi ya corona kamwe haikuwa kauli ya kupuuza kanuni za kisayansi za mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Akitoa salam za shukrani kwa Mungu na Watanzania kwa niaba ya Rais Dk. Magufuli ikiwa ni hitimisho la siku tatu za kumshukuru Mungu,baada ya maambukizi ya virusi vya corona kupungua nchini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano Dayososi ya Dar es salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi alisema licha ya kauli ya rais kutaka Watanzania kusali, bado Serikali ilisisitiza kufuatwa kwa kanuni za kisayansi za kuepuka maambukizi, ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa,kunawa mikono na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima. 

 Alisema hatua kufunga maabara yake iliyokuwa ikipima virusi vya corona kabla ya Rais Magufuli kubaini kasoro katika maabara kuu,hatua hiyo iliifanya Tanzania kuchukua hatua ya kujijengea uwezo wake wa ndani na kujenga maabara mpya yenye uwezo wa kuwapima watu wanaodhaniwa kuwa na virusi vya corona maradufu.

Alisema kupitia kwa waumini wa kanisa hilo, Rais Dk. Magufuli anashukrani kubwa sana kwa Mwenyezi Mungu na kwa Watanzania wote kwa kuitikia wito wake wa wananchi kuondokana na hofu, badala yake wamlilie Mungu jambo ambalo maombi hayo yamejibiwa kwa kupungua maambukizi.

Akizungumza wakati wa mahubiri, Canon Francis Xavery alimshukuru Rais Dk Magufuli kwa uamuzi wake wa kutofunga nyumba za ibada, ikiwemo makanisa na misikiti, licha ya mashinikizo kutoka sehemu mbalimbali jambo lilimfanya mwenyezi Mungu kusikia maombi ya Watanzania kwa kuwa walimwamini Mungu.

Padri Jacob Kahemele wa kani hilo, alisema kanisa hilo limeungana na waamini nchini kote kuitikia rai ya rais, huku akiwataka Watanzania kuacha kujipa hofu hususani katika mambo ambayo yanapita upeo wa binadamu,badala yake kila mmoja kwa imani yake kujinyeyekeza mbele ya Mungu ambaye ni suluhisho la mambo yote yanayoonekana na yasiyoonekana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles