27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wahudumu wa afya wasitisha mgomo

NAIROBI, Kenya 

WAHUDUMU wa afya nchini Kenya, wamesitisha mgomo wao ambao ulipangiwa kuanza jana kwa siku 21 kwa kile walichosema ni kutoa nafasi kwa mazungumzo baina yao na Serikali.

Wakizungumza  wanahabari juzi, Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi (KNUN), Seth Panyako na mwenzake wa Chama cha Maofisa wa Kliniki (Kuco), George Gibore walisema hatua hiyo imechochewa na changamoto zinazolikabili taifa hili.

Panyako aliongeza wahudumu wa afya wangesusia kazi kungetokea shida nyingi zaidi katika sekta ya afya wakati huu ambapo janga la corona, limesababisha shida nyingi kwa uchumi kando na masaibu yanayosababishwa na mafuriko.

Alisema mgomo utakuwa hatua ya mwisho endapo matakwa yao hayatashughulikiwa.

“Tunatoa wito kwa wahudumu wa afya kote nchini waripoti kazini kama kawaida, wakisubiri mwelekeo kutoka kwa uongozi wa vyama hivyo. Ijumaa wiki jana tulifanya mazungumzo na Wizara ya Afya na tukatambua masuala yote ambayo yamekuwa yakitutatiza katika siku chache zilizopita.

“Kama taifa wakati huu tunakabiliwa na shida nyingi; mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 200 na kuna uvamizi wa nzige kando na janga hili la Covid-19,” alisema.

Mapema  mwezi huu, wafanyakazi wa afya walitoa ilani ya mgomo wakitaka marupurupu yao ya kufanya kazi katika mazingira hatari yasawazishwe na wapewe vifaa tosha vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona (PPE).

Pia walilamika  hakuna mafunzo maalumu ambayo wamepewa kuhusiana na vita dhidi ya virusi vya corona, huku wakitaka mazingira yao ya kufanyia kazi yaimarishwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles