25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Ardhi kuanzisha masjala ya kisasa

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAM

WIZARA wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepokea vifaa kwa uanzishaji wa masjala za kutunza nakala za hati za umiliki wa ardhi, ikiwa sehemu ya urasimishaji wa makazi unaofanyika nchi nzima.

Vifaa vilivyotolewa ni kompyuta tano na mashine mbili za uchapishaji wa nyaraka mbalimbali za urasimishaji wa makazi.

Akizungumza wakati wa tafrija fupi ya kukabidhiwa vifaa hivyo katika ofisi za Ardhi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema kuwa uanzishwaji wa masjala hizo ni sehemu ya utakelezaji wa maelekezo ya Rais Dk. John Magufuli aliyeagiza Wizara ya Ardhi kuondoa kero zote za ardhi zinazowakabili wananchi.

“Niwashukuru Benki ya Maendeleo ya TIB ya kuunga jitihada za kuanzisha masjala hizi ambazo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais, hivyo zitasaidia kupunguza kero za Watanzania wanaposhughulikia masuala ya umiliki wa ardhi,” alisema Lukuvi.

Alisema kuwa lengo la urasimishaji ni kuhakikisha usalama wa miliki na kuwezesha upatikanaji wa maeneo kwa huduma za kijamii na miundombinu kwa njia shirikishi.

Aliongeza kuwa kazi hiyo itasaidia mzunguko wa fedha na kuimarisha uchumi kwa kuwa utasaidia wananchi kutumia nyumba zao kama dhamana ili kuweza kukopa katika taasisi za kifedha, pia litasaidia kuzipa fursa taasisi hizo kuweza kuhakiki umiliki wa waombaji wa mikopo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mipango, Mikakati na Uhusiano wa Kitaasisi za Benki ya Maendeleo ya TIB, Patrick Mongella, alisema kwa kiasi kikubwa taasisi za kifedha zinaitegemea Wizara ya Ardhi kwa utoaji wa mikopo kwa watu na taasisi mbalimbali ambao wanatumia ardhi kama sehemu ya dhamana ya mikopo yao.

“Zoezi hili ni muhimu kwa taasisi za fedha ikiwemo TIB kwa kuwa kwa kiasi kikubwa shughuli za ukopeshaji zinatumia ardhi kama sehemu ya dhamana ya mikopo,” alisema Mongella.

Aliongeza kuwa TIB kama benki ya Serikali iliona ni fursa nzuri ya kuunga mkono jitihada za wizara hili kuisaidia katika uwekaji wa kumbukumbu katika urasimishaji wa ardhi.

Alisema suala la urasimishaji wa makazi linahusisha kutambua, kupanga, kupima na kumilikisha maeneo yaliyoendelezwa bila kupangwa. 

Hivi karibuni akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi kwa mwaka wa fedha 2020/21, Lukuvi alisema katika kipindi cha miaka mitano wizara yake imeweza kuidhinisha michoro ya mipangomiji ya urasimishaji yenye viwanja 703,836.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles