28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Asilimi 66 ya wagonjwa JKCI wakutwa na shinikizo la damu

Mwandishi Wetu- Dar es Salaam

TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) tangu ilipoanzishwa mwaka 2015 hadi Aprili, mwaka huu, kati ya wagonjwa 334,774 iliyowatibu,  asilimia 66 ya wagonjwa  walikuwa na tatizo la ugonjwa wa shinikizo la juu la damu

Taarifa iliyolewa kwa vyombo vya habari na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Taasisi hiyo, Anna Nkinda Dar es Salaam jana, ilisema ugonjwa wa shinikizo la juu la damu hutokea wakati nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya moyo kuwa  kubwa kuliko kawaida. 

Taarifa hiyo, ilisema jana Tanzania iliungana na mataifa mengine duniani kuazimisha siku ya shinikizo la juu la damu duniani.

“Ongezeko hilo husababisha moyo kufanya kazi kupita kiasi ili kusukuma  damu katika mishipa ya damu. 

“Kwa kawaida ugonjwa wa shinikizo la damu halina dalili, ila likidumu kwa muda mrefu bila tiba lina madhara makubwa kiafya,”ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, ilisema kuna aina mbili za  ugonjwa wa shinikizo la juu la damu ambazo ni  shinikizo la juu la damu la kurithi na shinikizo la damu linalosababishwa na magonjwa mbalimbali. 

“Asilimia 95 ya wagonjwa  wa shinikizo la juu la damu hawana sababu inayoweza kujulikana kisayansi.

“Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu halina sababu inayoeleweka na mara nyingi inaweza kusababishwa na mgonjwa kuwa na historia ya ugonjwa katika familia yao, uzito mkubwa kupindukia, matumizi ya chumvi nyingi, kutofanya mazoezi, uvutaji wa sigara, ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na umri mkubwa,”ilisema taarifa hiyo. 

Asilimia kubwa ya watu wanaopata  ugonjwa wa shinikizo la juu la damu huwa katika kundi hili na magonjwa mbalimbali kama  figo, mishipa ya moyo na  mfumo wa homoni. Aina hii ya shinikizo la juu la damu  huathiri asilimia 5 ya wagonjwa wenye  shinikizo. 

Kwa mfano aina hii ya shinikizo la damu huweza kuwatokea kinamama  wakati wa ujauzito  na hupona  mara baada ya kujifungua.

Taarifa hiyo, ilisema ugonjwa  huo unaweza kusababisha mwili kupooza,kiharusi (stroke), shambulio la moyo (heart attack), moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure), kufanya moyo kuwa mkubwa, ugonjwa  wa figo na kupunguza nguvu za kiume.

Lakini taarifa hiyo, ilisema ili kuepuka kupata ugonjwa wa shinikizo la juu la moyo kwa kufanya mazoezi,  kuzingatia  lishe bora kwa kula  matunda, mboga mboga, vyakula vyenye madini ya potassium vile vile kupunguza kula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha mafuta  na chumvi. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles