31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MOI yatoa mafunzo kujikinga corona

Aveline Kitomary, Dar es salaam

TAASISI  ya Tiba ya Mifupa (MOI), imetoa mafunzo ya namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa wenyeviti pamoja na makatibu wa mashina ya chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Kisukuru,Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI,Dk.Boniface Respicious  alisema mafunzo hayo yamefanyika kutokana na ombi la viongozi wa Kisukuru ambao waliomba taasisi ya hiyo kutoa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo na uwelewa viongozi hao ili wakawaelimishe wananchi wao.

“Tulipokea mamombi ya kuja kutoa elimu hapa, tukaona tuje kwani jukumu letu ni kutibu na kuelimisha, tumewapa elimu kuhusu ugonjwa wa corona,tumewatoa hofu kumekua na uzushi mwingi kwenye miatandao ya kijamii,”alisema.

Alisema Serikali imefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya nchini,wananchi wasiwe na na wasiwasi kwani vifaa vyote vipo na ni vya kisasa.

“Kuna uzushi mwingi kwenye mitandao kwamba hapa nchini kuna ‘ventilator 2’ habari hizo ni uzushi mtupu na nawaomba mzipuuze, pale Muhimbili ,MOI, JKCI tunazo zaidi ya 99 ambazo ni za kisasa kabisa ambazo zimenunuliwa na Serikali yetu tukufu,” alisema.

Mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM Kata ya Kisukuru, Thomas Haule aliishukuru Serikali kwa jitihada kubwa za kupambana na ugonjwa wa Corona ambapo wananchi wamekua wakipata elimu na taarifa mbalimbali kuhusu ugonjwa huo.

” Nakushukuru mkurugenzi kwa kuja kutupa elimu, tumeelimika na elimu hii itawanufaisha wananchi wetu wote wa kata hii ya kisukuru, tunashukuru Serikali yetu ina watendaji ambao wanashuka mpaka chini, hatukutegemea kama mkurugenzi kutoka MOI, angefika hapa, amekuja na ametupa elimu,” alisema.

Mkazi wa Kata ya Kisukuru,Odacks Pembe alishukuru kwa mafunzo waliyopata na kuahidi kuendelea kuchukua tahadhari ili kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa corona.

“Serikali kupitia Wizara ya Afya imekua inafanya kazi nzuri na sisi wananchi tunashukuru sana kawani tunapata elimu, taarifa lakini pia huduma kwenye hospitali zetu ni nzuri, sisi wakazi wa Kisukuru tunaunga mkono jitihada za Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli na tuko naye bega kwa bega” Alisema Pembe

Mkufunzi kutoka MOI ,Georgina Chirwa aliwaasa wananchi wa kisukuru kufuata maelekezo yote yanayotolewa na Wizara ya Afya ikiwemo kuepuka mikusanyiko, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka na kuvaa barakoa na endapo mtu ataona dalili kupiga simu no 199.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles