25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yaahidi kutikisa

Na WINFRIDA MTOI – DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga, imewataka mashabiki wake kukaa tayari kupokea burudani zaidi katika mechi zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara.

 Ligi Kuu ambayo imesimama tangu Machi 17, mwaka huu, baada ya Serikali kupiga marufuku mikusanyiko ya watu ikiwemo michezo, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka maambukizi ya vizuri vya corona.

Hivi karibuni Rais Dokta John Magufuli, alisema anafikiria kuruhusu ligi kuendelea, lakini kwa sharti la mechi kuchezwa bila mashabiki.

Hadi ligi hiyo inasimama, baadhi ya timu zimecheza mechi 28, nyingine 29, huku Yanga pekee ikiwa imecheza michezo 27 na kukamata nafasi ya tatu, baada ya kukusanya pointi 51.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Mhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz, aliwataja mashabiki wao ‘kukaa mkao wa kula’, kwani kikosi chao kitarejea na makali zaidi.

Alisema kuwa, kutokana na mazoezi wanayofanya wachezaji wao, anamini watacheza mpira wa burudani na ufundi sambamba na kushinda michezo.

“Ninachopenda kuwaambia mashabiki wa Yanga, wakae mkao wa kupokea burudani, unajua kulikuwa hakuna mechi yeyote inayochezwa, kila mmoja ana hamu ya kuona timu yake inakuja vipi.

“Sisi Yanga tunasema tunarejea kivingine, tutacheza mchezo mzuri, yaani ‘softball, tunataka kila mmoja afurahi, pia tunaingia uwanjani kupambana kutafuta pointi 30,”alisema.

Alieleza kuwa, pamoja na kupigania nafasi mbili za juu, watapambana kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania maarufu Kombe la Azam.

“Wachezaji wetu tunawafuatilia, wazingatie program wanazopewa na mwalimu, pia wazingatie suala la afya katika kipindi hiki cha  ugonjwa wa corona,” alisema Nugaz.

Kuhusu suala la usajili, alisema kila kitu kinaendelea kulingana na mahitaji ya mwalimu, wakati ukifika wataweka wazi wachezaji waliowasajili lakini kwa sasa  wanajipanga na mechi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles