29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Dortmund yaitandika Schalke Bundesliga ikirudi

MUNICH, Ujerumani

LIGI Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, iliyosimama kwa takribani siku 65 kutokana na janga la virusi vya corona, ilirudi kwa kishindo jana huku mabao 12 yakifungwa ikiwemo ushindi wa mabao 4-0 ambao Borussia Dortmund walipata dhidi ya Schalke 04. 

Ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili msimu huu baada ya ule wa kwanza kumalizika kwa timu hizo kutofungana, mtanange huo ulimalizika kwa Dortumund kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0, wafungaji wakiwa ni Earling Braut Haaland (dk.29), Raphael Guerreiro (dk.45 na 63), na Thorgan Hazard (dk.48).

Kipigp hicho kinawafanya Schalke kuendelea kubakia katika nafasi ya nane kwenye msimamo wakati Dortmund wakiwa nafasi ya pili kwa pointi 54 wakizidiwa pointi moja na vinara Bayern Munich ambao leo wanamenyana na Union Berlin.

Aidha, kiboko ya vigogo Bundesliga, RB Leipzig walipepetana na Freiburg lakini walilazimika kusubiri hadi dakika ya 77 kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji raia wa Denmark mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen, hivyo timu hizo kugawana pointi kwa sare ya 1-1.

Katika mchezo mwingine ya mapema jana, mabao ya Renato Steffen na Daniel Ginczek yaliiwezesha Wolfsburg kurudi nyumbani na pointi tatu kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wao, Augsburg.

Ilikuwa ni siku nzuri pia kwa Hertha Berlin kwani licha ya kuwa ugenini waliweza kuzikusanya pointi tatu kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Hoffenhem.

Kwingineko, timu inayoburuza mkia, Paderbon, iliweza kuambulia suluhu ikiwa ugenini dhidi ya Dusseldorf, ambayo pia iko kwenye hatari ya kushuka daraja ikiwa inashika nafasi ya 16.

Mchezo wa mwisho kwa jana ni ule wa usiku uliowakutanisha wenyeji Frankfurt, ambao wako nafasi ya 12, na Borussia Monchengladbach iliyoko juu yao kwa tofauti ya pointi 11.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles