29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanafunzi ahamishwa shule baada ya kumpa ujauzito mwenzake

Khamis Sharif -Kusini Unguja

UONGOZI wa Shule ya Sekondari  Paje Wilaya ya Kusini Unguja, umemuhamisha shuleni hapo mwanafunzi wa kiume ambaye anadaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake.

Akithibitisha uhamisho wa mwanafunzi huyo, mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Issa Abdallah Makame alisema kuwa uongozi huo umeridhia hatua hiyo kwa lengo baada ya kuona ukubwa wa tatizo hilo shuleni hapo.

Alisema suala la wanafunzi kumpa ujauzito katika mazingira ya shule hiyo ni geni hivyo, uongozi umefanya uamuzi huo mgumu iki kutaka kuona matendo hayo hayajirejei tena kwa wanafunzi shuleni hapo.

Alisema kuwa mwanafunzi huyo ambae jina lake limehifandhiwa anasoma kidato cha nne  na tayari ameshapewa taarifa za kutafuta skuli nyengine ili kuendelea na masomo yake mara shule  zitakapofunguliwa.

Aidha mkuu huyo wa shule alisema kuwa mwanafunzi huyo anadaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake ambae anasoma kidato cha tatu shuleni hapo.

“Tulichokifanya kwanza ni uchunguzi yakinifu na ndipo tukaamua kukutana na kukubaliana tumpe uhamisho na ulikuwa tumpunzishe moja kwa moja lakini kwa vile karibuni anafanya mtihani ni bora aende akamalizia katika skuli nyingine kwani kuendelea kubakia hapa kutawafanya na wengine kuiga na kuishi kwa woga.

“Hii ni hukumu yetu kama shule tu, bila shaka kuna hukumu nyingine ya familia ya mtoto wa wa kike huko sijui itakuwa ipi kwani sio suala rahisi mzazi kufanyiwa mtoto wake kitendo kama hiki kisha wakamuangalia tu,” alisema Mwalimu Abdallah

Alisema tukio hilo ni la kwanza kwa wanafunzi kupeana ujauzito lakini wameona ni bora kuchukua hatua haraka ili wengine wasireje.

Akizungumzia hilo, Mratibu wa Wanawake wa Shehiya ya Paje, Asya Mussa Dai, alisema kuwa uamuzi waliochukuliwa na uongozi wa shule si mbaya kwani litakuwa fundisho kwa wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles