Na Elizabeth Kilindi -NJOMBE
JESHI la polisi mkoani Njombe, linawa- shikilia watu 13 kwa tuhuma za mauaji ya wanafunzi wawili wa familia ya Frank Chaula inayoishi katika Kijiji cha kipen- gere wilayani Wanging’ombe mkoani humo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Hamisi Issa, alisema watuhumi- wa hao wengine walihusika kukaa kikao cha kupanga njama za mauaji ya Chaula na watoto wake.
Alisema watuhumiwa hao waliua
watoto wawili wa Chaula ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha kuweka Akiba na kukopa, Saccos ya Kipengere waliokuwa wamelala kwenye nyumba ambayo pia hutumika kama sehemu ya duka la biashara.
Kamanda Issah alisema watu wanne watawaachia na kutokana na maelezo yao kuonyesha hawakuhusika na tukio la mauaji huku wengine wakitarajia kupandisha kizimbani hivi karibuni.
“Kuna watu 13 walikatwa kwa ajili ya mahojiano, wanne tunawaachilia, wengine watashitakiwa na kwa kesi ya mauaji na kuna wengine watashitakiwa
kwa kula njama ya kutekeleza mauaji,” alisema Kamanda Issah.
Alisema kabla ya mauaji hayo kufanywa kuna vikao vilikaa na vikaazi- mia lazima Chaula aweze kuondolewa duniani, lakini waliotekeleza mauaji wakaua watoto.
Alisema jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio la mauaji hayo. Mauaji ya Fabio Chaula ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa chuo cha uha- sibu jijini Dar es Salaam na Frank Chaula mwanafunzi wa Kidato cha nne sekond- ari ya Mount Kipengere lilitokea April 27, mwaka huu katika kiiji cha Kipengere