32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

CT Scan Muhimbili yagharimu Sh bil 3.5

ct scanNa Veronica Romwald,  Dar es salaam

SERIKALI imefunga mashine mpya ya CT Scan yenye gharama ya Dola za Marekani  milioni 1.7 ambazo ni  sawa na zaidi ya Sh bilioni 3.5 katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Mashine hiyo,  yenye uwezo wa kupiga picha zaidi ya 128 kwa wakati mmoja, ikilinganishwa na iliyokuwapo awali ambayo ilikuwa inapiga picha sita kwa wakati mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini wake, Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangwala, alisema mashine hiyo itakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi ambao walikuwa wanakosa huduma hiyo.

Alisema Serikali imeamua kufunga mashine  mpya kwa sababu ya awali imekuwa ikiharibika mara kwa mara na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa.

“Nashukuru maagizo yaliyotolewa yametekelezwa katika kipindi kifupi, hii inadhihirisha tukishirikana kwa namna hii tutatoa huduma bora kwa Watanzania, tumeanza hapa Muhimbili tutakwenda hospitali zetu za Dodoma na Mwanza, ” alisema

Alisema ufungaji wa mashine  ya CT-Scan, ni hatua nzuri kwa serikali ya awamu ya tano na kwamba wamejipanga kufanya mambo makubwa.

Alipotembelea  jengo la Mwaisela,alishuhudia kitengo cha kulaza wagonjwa mahututi (ICU) ya kisasa ambayo imeanza kuwekewa vifaa.

Dk.Kigwangwala, alimtaka Kaimu Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru na watendaji wengine kuboresha utoaji wa huduma ili kuwavutia watendaji walioko chini yao.

“Lazima huduma ziboreshwe ili kuwavutia hata wale wanaokwenda kuhudumiwa katika vituo vya watu binafsi…nauagiza Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya  (NHIF) kuondoa Muhimbili katika kundi la pamoja na hospitali nyingine kuanzia sasa, kwani haina hadhi sawa na zingine. Hapa tunatoa huduma si kutaka fedha za wagonjwa,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles