24.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Ummy: Wahudumu wa afya msiwakimbie wagonjwa

Nora Damian Na Aveline Kitomary -Dar es salaam

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amewataka wahudumu wa afya kutokuwakimbia wagonjwa kwa hofu ya kuambukizwa magonjwa na badala yake wafuate kanuni na miongozo iliyopo katika kujikinga.

Ummy alitoa rai hiyo jana wakati akipokea msaada wa vifaa vya kunawia mikono 100 vyenye ujazo wa lita 500 kutoka kwa Shirika lisilo la kiserikali la Water Mission Tanzania.

Alisema kama mtaalamu wa afya atafuata mwongozo wa kuzuia maambukizi wa mwaka 2018  na mwongozo wa uzuiaji wa maambukizi ya virusi vya corona (Covid-19), hataweza kupata maambukizi kutoka kwa mgonjwa.

 “Wakati tunaendelea kukabiliana na janga la ugonjwa wa Covid-19, tukumbuke kuwa kuna magonjwa mengine kama ya moyo, kisukari, malaria, figo na ya kuambukiza ikiwemo Ukimwi na kifua kikuu.  

“Hivyo basi mgonjwa wa aina hii akifika katika kituo cha kutolea huduma za afya anatakiwa kutibiwa na siyo kukimbiwa.

“Baadhi ya wahudumu wakimpokea mgonjwa mwenye joto kali wanamkimbia kwa kudhani kuwa ana ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona. 

“Mwongozo wa utoaji wa huduma za afya hauwataki kuwakimbia wagonjwa, jambo la muhimu ni kufuata miongozo iliyopo hii ikiwa ni pamoja na kunawa mikono, kuvaa barakoa na glovu wakati unamuhudumia mgonjwa,” alisema Ummy.

Alishukuru msaada uliotolewa na Water Mission Tanzania na kuwataka wananchi kuzingatia maagizo wanayopewa na wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni pamoja na kuvaa barakoa katika kukabiliana na ugonjwa wa corona.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Water Mission Tanzania, Benjamin Filskov, alisema taasisi yake imetoa msaada huo wa vifaa ambavyo vitatumika katika vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Abubakar Khunenge, alisema watahakikisha vifaa hivyo vinatumika kama ilivyokusudiwa katika kupambana na maambukizi ya Covid-19.

“Tutahakikisha vifaa hivi vinapelekwa katika vituo vya kutolea huduma za afya vilivyokusudiwa na vitawekwa katika mlango wa mbele wa kuingilia katika kituo husika,” alisema Khunenge.

TAHARUKI AMANA

Katika hatua nyingine, taharuki imezuka katika Hospitali ya Rufaa Amana iliyopo Manispaa ya Ilala baada ya baadhi ya wagonjwa wa corona waliokuwa wamelazwa kutaka kuondoka kwa madai wanajisikia vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles