26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Upelelezi kesi kigogo Takukuru wafika pazuri

Kulwa Mzee -Dar es Salaam

UPELELEZI wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa zamani wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kulthum Mansoor uko katika hatua nzuri.

Lakini shauri limeshindwa kuendelea kwa sababu hakimu anayesikiliza kesi hiyo ana udhuru.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Vick Mwaikambo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa na upelelezi upo hatua nzuri.

Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya ambaye ana udhuru, hivyo aliomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa kutajwa.

Shauri hilo namba 26/19 lilisikilizwa kwa njia ya video conference.

Kulthum anawakilishwa na Wakili Elia Mwingira na anakabiliwa na mashtaka   manane ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha Sh bilioni 1.477.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 2013 na Mei 2018, mshtakiwa alighushi barua ya ofa ya Agosti 13, 2003 kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa imetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, huku akijua kuwa si kweli.

Katika shtaka la pili, inadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017, maeneo ya Upanga ndani ya Wilaya ya Ilala, mshtakiwa kwa kudanganya alijipatia Sh milioni 5.2 kutoka kwa Alex Mavika ambaye ni mfanyakazi wa Takukuru kama malipo ya kiwanja kilichopo Kijiji cha Ukuni, Bagamoyo.

Pia inadaiwa kati ya tarehe hizo,  Kulthum alijipatia Sh milioni tatu kutoka kwa Wakati Katondo kama malipo ya kiwanja kilichopo maeneo ya Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Mshtakiwa anadaiwa alijipatia Sh milioni 5 kutoka kwa ofisa wa Takukuru, Gogo Migutah kama malipo ya kiwanja kilichopo eneo hilo hilo.

Katika shtaka la tano, inadaiwa Kulthum alijipatia Sh milioni 7 kutoka kwa Ekwabi Majungu ambaye pia ni ofisa wa Takukuru kama malipo ya kiwanja hicho.

Kulthum anadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017, maeneo ya Upanga, Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathminu alijipatia Sh milioni 7 kutoka kwa John Sangwa kama malipo ya kiwanja cha eneo hilo.

Inadaiwa mshtakiwa akiwa mwajiriwa wa Takukuru, alijipatia Sh milioni 5 kutoka kwa Rose Shingela kwa malipo hayo.

Katika mashtaka ya utakatishaji fedha,  inadaiwa kati ya Januari 2013 na Mei 2018, maeneo ya Upanga, mshtakiwa  alijipatia Sh 1,477,243,000 wakati akijua fedha hizo ni haramu na ni zao la kosa tangulizi la kughushi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles