29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Lipuli kuendelea kuukosa mtambo wa mabao

Winfrida Mtoi, Dar Es Salaam

STRAIKA wa Lipuli FC, Daruwesho Saliboko, ataukosa mchezo dhidi ya Ndanda FC, unaotarajia kupigwa leo  Uwanja wa Samora, Iringa.

Nyota huyo anauguza jeraha la goti, baada ya kuumiwa wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons, uliochezwa Februari 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya

Katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Saliboko anashika nafasi ya nne, akiwa na mabao nane.

Kinara wa vita hiyo ni mshambuliaji a Simba, Meddie Kagere aliyetikisa nyavu mara 14.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha Msaidizi wa Lipuli, Julio Elieza, alisema kumkosa mchezaji huyo ni pigo kubwa kwao katika kipindi hiki wanachohitaji kujinasua kutoka nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Alisema mbali ya Saliboko, kikosi chake pia kitamkosa beki, Novart Lufunga, ambaye anauguza jeraha la goti, hatua itakayomfanya kuwakosa wachezaji wake wawili muhimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles