24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

wanaoshtakiwa uhujumu uchumi waomba kurejeshewa kadi za benki

Kulwa Mzee -Dar Es Salaam

VIGOGO wawili wa uthamini wa madini ya almasi wa Serikali, wanaoshtakiwa kwa uhujumu uchumi, wamewasilisha maombi kwa kiapo wakitaka mahakama iamuru warejeshewe kadi zao za benki.

Wathamini hao, Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania  (Tansort) Archard Kalugendo na Mthamini almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini waliwasilisha maombi yao kwa kiapo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akiiwakilisha Jamhuri mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, wanatoa maelekezo kwa wapelelezi ili kukamilisha katika maeneo machache yaliyobakia.

Wankyo aliifahamisha mahakama kuwa alipokea maombi kutoka kwa washtakiwa yaliyoelekezwa kwa mahakama kuomba warejeshewe kadi zao za benki.

“Mheshimiwa Hakimu, maombi yao wameyaambatanisha na hati ya kiapo, hivyo tunaomba muda wa wiki mbili ili tuwasilishe majibu kwa kiapo kinzani,” alidai Wankyo.

Upande wa utetezi haukuwa na pingamizi, kesi iliahirishwa hadi Machi 20 kwa kutajwa na maombi ya kadi za benki yatatajwa Ijumaa wiki hii.

Kalugendo na Rweyemamu wanasota mahabusu kwa miaka mitatu sasa  wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, wakidaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni  2.4.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wanakabiliwa na shtaka la kuisababishia Serikali hasara ya Sh  2,486,397,982.54 ambapo wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017 maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.

Washtakiwa wanadaiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao, wakiwa wathaminishaji wa almasi wa Serikali na waajiriwa wa wizara hiyo waliisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43  ambazo ni sawa na Sh 2,486,397,982.54.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles